Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limethibitisha kupokea maiti 22 za Waethiopia zilizosafirishwa kutoka mkoani Dodoma zilipokuwa zimehifadhiwa na kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti Mkoa wa Morogoro.
Maiti 42 zilikuwa zimehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti mkoani Dodoma na kutokana na idadi ya maiti kuwa kubwa ndipo zilipohamishiwa mkoani hapa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alisema wahamihaji hao kutoka nchini Ethiopia walikuwa wakielekea nchini Malawi ambapo walianza kufariki dunia wakiwa safarini huku wakiwa ndani ya lori.
Alisema Polisi wanamtafuta dereva wa lori hilo ambaye hajulikani alipo na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano punde watakapomwona mtu wasiyemfahamu katika eneo lao.
Shilogile alisema kwa sasa uingiaji wa wahamiaji haramu kutoka nchi za Ethiopia na Somalia umepungua kutokana na mikakati mbalimbali iliyofanywa na jeshi la polisi ikiwemo ya kufanya upekuzi katika vizuizi vyote vilivyopo katika mkoa wa Morogoro.
Aidha, amewaomba wananchi Morogoro hususani kwa zile wilaya za pembezoni kutoa taarifa mara moja katika vyombo vya sheria vilivyopo karibu pindi watakapoona watu wasio wafahamu.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment