TANZANIA INAWAHITAJI WATU WAKE KURUDI NYUMBANI KUIJENGA NCHI.
1. Kwa nini Watanzania wengi wanaoishi nje hawataki kurudi nyumbani japokuwa wamebanwa na Maisha ya huko?
2. Je huku ni kukwama au kukomaa?
3. Unawashauri nini wadau hawa?
Tafadhali elekeza majibu yako sehemu ya maoni. Tuanzie hapo kupata ufumbuzi wa kurekebisha mwelekeo wetu. Katika Tanzania ya sasa blogs zinaweza kufahamisha, kuelimisha na kukosoa jamii zaidi kuliko radio na tvs
Nianze na mawazo yangu mwenyewe;
- Ninadhani maisha ya nje ni vigumu sana kuweka akiba kutokana na utaratibu uliowekwa na nchi hizo. Mfano USA, Australia, UK na nchi zote za magharibi utaratibu ni kufanya kazi na kipato kwa wageni wengi ni kutosha kununua chakula na mavazi, kulipa kodi ya nyumba, kulipa bills na kukidhi mahitaji mengine ya lazima ya maisha, hivyo hakitoshi kuweka akiba.
- Muda unakimbia kama kishada, umri unapepea, wengi wao wanaona hakuna maendeleo yeyote kinyume na matarajio kwa hiyo watanzania wengi wananunua muda. Kurudi nyumbani bila kitu maalum cha kufanya ni kupingana na mpango mzima uliowafanya kwenda nchi hizo, kwa hiyo wanakomaa. Japo mwisho haujulikani.
- Ushari wangu; kila kitu kinawezekana. Njia pekee ya kujikwamua kusudi kurudi nyumbani, kuondokana na woga wa maisha ni kushirikiana(makundi) kusudi kupata akiba na kila kundi kutumia akiba hiyo kuwekeza nyumbani kusudi kujiajiri wenyewe na kisha kurudi nyumbani kwa utaratibu na mpango ulionyooka.
9 comments:
Mimi binafsi naogopa ugonjwa wa malaria na majambazi. Usiku unapoingia nakumbwa na wasiwasi wa kug'atwa na mbu na hofu ya kuingiliwa na majambazi. Kama serikali itakomesha vitu hivyo viwili leo, kesho naondoka kurudi. Lakini pia kuna watu ambao wameukana utanzania na kuwa raia wa Marekani. Sasa kuwambia warudi nyumbani sijui una maana gani, kwa sababu wao tayari wapo nyimbani. Tanzania ni ugenini.
Haya Mdau, there you go again na maswali yako ya chuo kikuu.
Jibu langu kwa swali lako la kwanza; Ni kwamba hakijaeleweka na hakieleweki. Shule hazimalizikiki, kazi/schedule tunazofanya malipo yake hayatoshi kukidhi hata mahitaji uliyoyataja. Hakuna mtu anayetaka kurudi bongo kuchekesha.
Jibu la swali la pili; nadhani hii ni dalili ya kunasa yaani ni zaidi ya kukwama, na siyo kukomaa. Maana ya kukomaa iko siku mambo yatakuwa mazuri.
Ushauri kwangu na wengine ni sawa na mdau tuanze utamaduni wa kushirikiana kusudi kupunguza matumizi tuweze kufanya saving, je lakini hicho kitu kinawezekana miongoni mwa Watanzania? Hichi ni kitendawili.
naona wewe muandishi unamlengo wa upande moja inabidi uelewe sometimes being in european countries including usa and canada sio tu tunahitaji kuitoa bali ni maisha yote yanayokuzunguka yanakufanya uone ni bora kuishi nje kuliko home,pia if u go by percentage im sure majority kwa namna moja au nyingine wapo bora nje kuliko nyumbani except kwa watoto na wale waliokuwa wanaishi na MAFISADI,NA NINADHANI DHINA DHIMA NZIMA YA HUU UJUMBE UNAWALENGA ASSOCIATE OF MAFISADI ,KWANI HAWANA SABABU YA KUJA ULAYA IKIWA ULAYA WAMEIACHA MAJUMBANI KWAO
Wengi (nikiwemo) wanaogopa kwenda jela kwa kuwa ukishaishi nje, nchi kama Marekani ukiona wanavyotumia pesa za walipa kodi kwa adabu ya hali ya juu, kisha ukalinganisha na bongo, lazima utapandwa na hasira, utawasemea watu ovyo kisha uishie lupango. Kuliko nikapandwe na hazira niende keko bora nibanane huku huku. Mbu kwa watu wengi siyo tatizo mpango wa kuwatokomeza unawezekana. Off-course wenzetu kwao kuzuri kwa kuwa wamekutengeneza, lakini kwetu kunawezekana kutengenezwa? Kila mtu aambiliki, na kila mtu anataka kujinufaisha binafsi kupitia mali za umma. Unasemaje kuhusu hili mdau uliyoanzisha mjadala huu?
mdau, RUSHWA ikiisha niambie niatarudi mbio. kwa sasa Im better here, wayyyy much better
Hahahaahhaaha Kazi kwelikweli!!!!!
mimi binafsi niko hoi bin taaban nataka kurudi nyumbani lakini siwezi because sijajiwekea kitu nyumbani so kwa muda wote nilipo huku nikirudi home patumu ni noma kiyama so bora nikomaa huku huku na huku huku pia hakieleweki because sina makaratasi ndu najiona kama niko jela lakini niko huru.
niombeni mungu anisaidiye amin.
kweli kabisa ndugu zangu, tuko better off huku kuliko nyumbani, rushwa, matajiri wengi waliupata kwa ufisadi na corruption,watu wahali ya chini ni shida tupu, kitu gani kitanirudisha nyumbani, kuja kuona watu wa hali ya chini wakifa kwa kushindwa kupata dawa hospitalini, huku uk, matibabu bure, shule bure, huwezi kufa njaa. Rushwe ikiisha ma mimi nitarudi, tanzania kusiwe na masikini wa tajiri
Mimi nafikiri mdau unapotafsiri maisha ya wote kwa muongozo wa maisha yako binafsi au ya wachache waliowako,sio sahihi.Na pia ungetanua swali lako na kulipa pande mbili. Kajaribu kwenda kutembea na wajuba wanuse kama upo mjini. wacha mtandao wa mafisadi, kuna mtandao wa majambazi na wa kila aina. Tumeridhika na maisha haya. ukifukuzwa kazi asubuhi, jioni umepata nyingine.
Post a Comment