Ulishawahi
kwenda kwa
semina au mkutano wa wafanyabiashara,wakati wa mapunziko au mwisho wakati wa
kubadilishana mawazo na kujenga mtandao zaidi wa kibiashara ukawa mkiwa(pekee
yako)?Haupo peke yako,watu wengi huwajisikii vema wakiwa ndani na watu
wasiowazoea/zoeana nao.Lakini matukio ya kutengeneza mitandao ya
kibiashara(networking business events) yanasaida sana kufanya biashara yako
kukua zaidi na pia yanakuwezesha wewe kufanya taifi za papo kwa hapo juu soko
lako.Kujifunza kujichanganya na watu nakufuatilia mawasiliano msilio badilishana
kwa matukio ya kibiashara ni muhimu sana
kwa mafanikio ya biashara yako sana sana kama mtu umejiajiri mwenyewe.Zifuatazo
ni dondoo ambazo zitakusaidia wewe kukuunganisha na wengine vema zaidi:
KABLA YA TUKIO
Jiandae kwa ajili ya tukio kwa kutengeneza business
card za kutosha,peni,kitabu kidogo(note-book).Hakikisha umekula kabla ya kwenda
tukio.Kama ni ni sherehe ya cocktail au chakula kinatolew/hudumiwa huko,wakati
wa kubadilishana mawazo na kutengeneza mtandao wako, ni bora ukakabeba kinywaji
tu pekee,kuliko kuzunguka na sahani ya chakula kila sehemu.
Elewa lengo
lako:Nini
nia yako ya kuhudhuria tukio husika?kukutana na watu Fulani?Kutafuta wateja
wako wapya watarajiwa?Kutafuta rasilimali unazohitaji?Kukutana na marafiki
wapya?Kukuza uhusihano ulipo wewe na wengine?
Mathalani
peleka business card 20 na hakikisha unazigawa kwa watu
zote kabla ya kuondoka.Ulizia pia
kwa watu wengine kama wana business card kama dhahiri unataka kuendelea
wasiliana nao.Sio kila mtu utakaye kutana naye atakuwa rasilimali kwako.
Ongea na
mwandaaji
wa tukio kuhusu vazi la siku hiyo(dress
code)Matukio mengine yanahitaji mtu uvae mavazi rasmi kimwonekano wa biashara
zaidi kama suti.Matukio mengine yanahitaji kuvaa mavasi yasio rasmi(kawaida), na mengine ni
mchanganyiko wa mitindo yote kutokana na
matakwa ya mtu binafsi.
Kwa kujua kwa
awali(kabla)
nini unatarajia ,unaongeza hamasa na hisia za kujisikia kuwa mmoja kati ya
kundi la tukio husika.
NDANI YA TUKIO
Kwanza wasili
mapema kwa tukio.Fika pale mapema sana wakati kundi likiwa dogo na nirahisi
kuongozeka.Ingia kwa bwalo/ukumbi kwa tabasamu.Hata kama unajisikia
vibaya/hasira siku hiyo igiza tu kama unafuraha kwa kuweka tabasamu kwa sura
yako utaoneka kwa wengine unaingilika,ni rafiki kwa kila mtu,unashauku la kufahamiana na wengine.Hakikisha
unajichanganya na wengine.Usijitenge na
kukaa na marafiki zako pekee au washirika wako unaowajua,tembea tembea .Tumia
sio zaidi ya dakika 5-6 kuzungumza na kila mtu.Wafikie watu mbalimbali na
jitambulishe kwa kila mtu(kama sio mmoja wa wana kundi,waombe kwanza wahusiki
ili wakuruhu kama unaweza kuwa mmoja wa wao,kisha wasalimie na kujitambulisha
kwao,inakupatia nafasi ya kufungua milango kwao)
Wakati
ukikutana na watu wasalimie kwa kuwashikana mikono na urudie majina yao,hii haisadii tu
kuyakumbuka majina yao ,bali inaonyesha uweka juhudi kusikia vema majina
yao.Vaa kikadi ambacho kinaonyesha jina lako na ukiweke mbele ya shati lako ili
kila mtu aweze soma vema jina lako,weka upande wa kulia wa bega lako ili iwe
rahisi kilamtu kukiona wakati ukishana nao mikono.Jifunze jinsi ya
kujitambulisha wewe mwenyewe,katika sekunde chini ya thalathini eleza kazi
yako.
Sikiliza zaidi
watu kuliko kuongea.Kumbuka hamna kitu bora zaidi
ya kusikila kimakini zaidi na kuonyesha
moyo wa kuwakubali watu wengine.Uliza swali na sikiliza majibu kimakini
sana ili uweze kumwelewa mtu.Hii itakusaidi kugundua mteja mzuri wa kufanya naye kazi kwa huduma au bidhaa zako.Chukua kumbukumbu ili
uweze kukumbuka nini watu wamesema.
Wakati ukirudi ofisini weka taarifa zote
katika program ya mawasiliana ya uongozi.
BAADA YA TUKIO
Baada ya kupata business card zao,ana kufuatilia
ndani ya masaa 24 baada ya tukio.Kama mnaweza kutengene muunganiko wenye manufaa kwa pande zote mbili ya
kibiashara na watu ambao mmekutana nao
kwa tukio,wapigie simu na kuwakaribisha kwa mlo wa mchana kwa ajili ya
kuendeleza zaidi muunganikao wenu wa kibiashara.
Kwenye kalenda
yako wakati
ukiandika semina au matukio unayotarajia kuhudhuria tenga pia masaa mawili au
tatu ya kesho yake kufuatilia ili uweze fanikisha kazi nzima.
Wakati ukiangalia matukio yajayo ya kibiashara yenye nia ya kutengeneza mitando
baina ya wafanya biashara,fanya tafiti za soko(market research) na ujue wateja
gani unatarajia kwenda kukutana nao,inaweza
ni bonge la furaha badala ya huzuni.Kupangilia kitu kinakufanya wewe
ufanye vema zaidi.
Author:Deogratius kilawe
Title:Business consultant
Phone:+255717109362
Email:deogratiuskilawe@yahoo.com
Blog:Tanzaniaachievers.blogspot.com
Facebook/Skype ID:Deo kilawe/Kilawe 1
No comments:
Post a Comment