Advertisements

Tuesday, June 5, 2012

MWANAHABARI ATHUMAN HAMIS ANAOMBA MSAADA WENU

Bw. Athuman Hamis ambaye ni Mpiga Picha wa magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspaper (Sunday News, SpotiLeo, Daily News na Habari Leo) akiongea na waandishi wa habari leo juu ya mustakabali wa maisha yake tokea amepata ajali ya gari.
Alisema kuwa, "Nimekuja leo kuutangazia Umma hali ilivyo. Ukweli kwa sasa account yangu ya CRDB ilikuwa maalum kwa ajili ya kusomeshea watoto, imekauka ya Postal Benki ambayo ni ya mshahara haina kitu. Pesa ya mshahara inayoingia benki ni 450,000/-
Namlipa nesi na msaidizi wake na mfanyakazi kiasi cha tshs. 370,000/-. Maisha ya ulemavu ni ghali sikutarajia. Nina wanangu watatu, wa kwanza anamaliza darasa la Saba mwaka huu, wa pili yuko la nne na wa mwisho yuko darasa la pili.
Hawa wanaosoma shule ya msingi niza kulipia 200,000/- kila term jumla 400,000/- hizo shule zina term nne kila mwaka. Gharama za chakula, vifaa vya wanafunzi, gharama zao ndogo ndogo na za kifamilia pamoja na chakula kwa mwezi, inakwenda kati ya 750,000/- mpaka 900,000/- kwa mwezi.
Nimekuwa omba omba mpaka watu kadhaa siwalaumu, wamechoka hawapokei simu wala kujibu sms. Siyo siri, ndugu wote wamekimbia waliobaki ni marafiki wa kweli wamenitangazia katika familia zao. Hali yangu ni mbaya sana kiuchumi.
Sina uwezo wa kulipia nyumba kwa gharama zozote zile. Mimi Athuman Hamis naomba Watanzania watakaoguswa wanisaidie. Kubwa ni nyumba na ushauri wa madaktari walionishauri nisiishi mbali na mazingira ya hospitali kulingana na hali yangu.
Makampuni, Mashirika, Wizara yoyote, Shirika la Nyumba la Taifa NHC, Watu binafsi, Serikali na Taasisi yoyote watakaoguswa na kilio changu nawaomba wanisaidie kwa njia yoyote. Kwa walio tayari naomba misaada ipitie katika account ya CRDB no; 01J2027048800 na Account ya Postal Benki no; 010-00090488.
Kwa wanaotumia mitandao ya simu wanaweza kutumia M-Pesa 0757825737Tigo Pesa 0655531188 naAirtel Money 0784531188. Au unaweza kumtumia rafiki yake Bw. Chris Mahundi M-Pesa 0767298888,Ephraim Mafuru Airtel Money 0686710977.

No comments: