ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 6, 2012

AJALI YA TRENI KITUO CHA WEST HYATTSVILLE

Kumetokea ajali ya Treni leo mida ya saa 10:45 jioni kwenye kituo cha West Hyattsville mabehewa matatu ya nyuma yalipotoka nje ya mataluma karibu na treni ilipokua inakaribia kuingia chini ya Ardhi kuelekea kituo cha PG.

Treni hiyo ilikua imebeba abiria takribani 55, hakuna liyejeruhiwa sababu za ajali bado kujulikana lakini wataalam wa mambo ya mataaluma wanasema joto linaweza kuwa sababu kubwa lililopelekea mataaluma kutanuka.

Kwa sasa usafiri wa Treni kutoka PG mpaka Fort Totten umesitishwa kwa muda badala yake yametolewa mabasi ya bure kutoka PG hadi Fort Totten.

No comments: