Chama Cha Mapinduzi (CCM) kesho, Jumapili, Julai 22, kinatarajiwa
kuutikisa mkoa wa Kigoma, kwa mkutano wake mkubwa wa hadhara,
utakaofanyika kwenye Viwanja vya Communicy Cetre mjini Mwanga mkoani
hapa.
Mkutano huo mkubwa umepangwa kuhutubiwa na
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye,
na baadhi ya mawaziri walioalikwa kueleza utekelezaji wa ilani ya CCM
katika sekta wanazohusika nazo.
Mkutano huo, umepangwa kuanza mapema kwa kuwa
unatakiwa kumalizika saa kumi jioni ili kuwapa fursa wananchi waliofunga
kwenda kufuturu baada ya kushinda ana swaumu ya Mwezi huu mtukufu wa
Ramadhani.
Awali Mkutano huo ulikuwa ufanyike, Ijumaa
iliyopita, lakini ukalazimika kusogezwa mbele baada ya taifa kuingia
katika maombolezo ya siku tatu, kufuatia ajali ya meli iliyotokea
Zanzibar ambapo watuzaidi ya 50 wamefariki dunia.
Katika mkutano huo wa kesho Jumapili, Nape na
baadhi ya mawaziri na manaibu mawaziri walioalikwa akiwemo Steven Wasira
na Aggrey Manri, wanatarajiwa kueleza utekelezaji wa Ilani ya CCM
mkoani Kigoma na Tanzania kwa jumla.
Pia wanatarajiwa kueleza sera za CCM, na kueleza
wananchi wa Kigoma, nini CCM imefanya, inafanya sasa na inatarajiwa
kufanya nini baadaye katika kukifanya chama hicho na serikali yake,
kuendelea kuwa makini na imara katika kuliongoza taifa la Tanzania.
Kufuatia mkutano huo kuahihirishwa karibu kona
zote za mji wa Kigoma na vitongoji vyake kama Ujiji, Kahabwa, Gungu na
Mwandiga, wamekuwa wakijadili kuhusu mkutano huo, kwenye vijiwe vya
kahawa, vituo vyua daladala na kwenye mikusanyiko hasa ya vijana, hamu
kubwa ikiwa ni kutaka kumsikiliza Nape na wabunge watakaopanda jukwaani
kwa mtindo wa aina yake.
Pia baadhi ya watu wameonyesha hamu ya kuhudhuria
mkutano huo kutokana na staili ambayo inaelezwa kuwa ni mpya na nzuri
ya CCM kuwapeleka kwenye mikutano ya hadhara baadhi ya mawaziri kueleza
wanavyosimamia utekelezaji wa ilani ya Chama kwenye sekta zao.
"Kwanza mimi ningependa nimsikie Nape, nasikia ni
msema kweli kama kuna jambo huwa hasiti kusema hata kujwaani, na pia
nitapenda niwasikie mawaziri watakaowaleta kwa sababu kwa muda mrefu
hatujawahi kumsikia hapa Kigoma waziri yeyote akisimama jukwaani kwenye
mkutano wa hadhara kueleza utekelezaji wa ilani", alisema Joseph
Chishako wa Mwandiga.
No comments:
Post a Comment