Mwanamuziki wa Rap wa Marekani Snoop Dogg amefungiwa miaka 2 kutoingia Nchini Norway baada ya kukamatwa akiwa amebeba bangi alipokua anaingia Nchini hiyo kuhudhulia tamasha la muziki lililofanyika mwezi June kusini mwa Norway..
Holger Hagesaeter wakili wa Norway aliyemuakilisha mwanamuziki huyo aliwaambia waandishi wa habari kwamba Snoop Dogg ambae jina lake kamili ni Calvin Broadus amekubaliana na uamuzi huo na wala hafikirii kukata rufaa.
Snoop Dogg aligundulika na bangi gram 8 baada ya mbwa wanaonusa mabeki uwanja wa ndege wa Norway alipong'ang'ania begi la mwanamuziki huyo pia Snoop alikua ameingingia na Cash nyingi kuliko inavyotakiwa.
Snoop Dogg alilipa faini ya Krona 52,00 sawa na dola 8,600
No comments:
Post a Comment