Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imesema ajali za meli zinazoendelea kutokea na kuua watu wengi zimesababishwa na soko huria la biashara katika sekta ya usafirishaji baharini visiwani humu.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed, wakati akifunga mjadala wa taarifa ya serikali kuhusu ajali ya boti ya MV Skagit iliyotokea Julai 18, mwaka huu.
Meli hiyo ilizama Bahari ya Hindi na kuua watu 114, wengine 146 kuokolewa na 30 kupotea.
Meli hiyo iliingizwa Zanzibar kutoka Marekani Oktoba, mwaka 2011 ikiwa imebakiza miaka miwili kumaliza muda wa matumizi.
Waziri Aboud, alisema tangu SMZ kuruhusu wa wafanyabiashara kuwekeza katika sekta hiyo, kumetokea wenye mitaji midogo ambao wamekuwa wakinunua meli chakavu (mitumba) na kutoa huduma visiwani hapa kutokana na kushindwa kumudu gharama za meli mpya.
“Uingizaji wa meli za mitumba chanzo cha ajali nyingi kwa sababu wafanyabiashara wengi wanashindwa kumudu gharama za meli mpya Zanzibar,” alisema.
Alisema kufuatia ajali hizo, serikali imeamua kuvizuia vyombo chakavu kufanya biashara katika eneo la mwambao wa Bahari ya Hindi visiwani humu.
Vile vile, alisema serikali imeamua kuvifanyia ukaguzi vyombo vyote vya usafiri baharini kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usafiri Nchi Kavu na Majini (Sumatra) Tanzania Bara.
Kwa mujibu wa waziri huyo, SMZ pia imeamua kuifanyia marekebisho makubwa Sheria ya Usafirishaji baharini Zanzibar ya mwaka 2006 ili kuhakikisha viwango vya ubora wa meli vinazingatiwa kabla ya kuingizwa nchini na kuanza kutoa huduma.
Katika mabadiliko hayo, alisema meli itakayosajiliwa Zanzibar, lazima iwe mpya au iliyotumika katika muda wa miaka 15 tangu kuundwa kiwandani.
“Hatutaki Zanzibar kugeuzwa dampo la meli chakavu na watu kupoteza maisha yao, " alisisitiza Waziri Aboud.
Aliongeza kuwa serikali hiyo imepiga marufuku boti na meli kufanya safari za usiku kutokana na sababu za kiusalama na kuonya kuwa meli itakayokiuka amri hiyo mmiliki wake atachukuliwa hatua na Mamlaka ya Usafirishaji Baharini Zanzibar.
Kwa upande mwingine, alisema serikali imepiga marufuku uuzaji wa tiketi nje ya vituo maalum na kuviagiza vyombo vya dola kuwakamata watakaokwenda kinyume na amri hiyo.
SMZ inajipanga kununua meli mpya na imekwisha kuzuia boti tatu kutoa huduma kutokana na sababu za kiusalama.
Boti hizo ni MV Karama, Mv Seagulla na Sephdeh, na meli ya MV Serengeti kupunguzia kiwango cha kuchukua mizigo na abiria kutokana na uchakavu na kuzima mara kwa mara baharini.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment