
“Mv Skagit ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 300 pamoja na mizigo tani 26, hivyo kulingana na idadi ya abiria 288 walioondoka katika chombo hicho isingeweza kuleta madhara kama hayo, ila tunawasiwasi waliongeza abiria njiani au mawasiliano ya hali ya hewa” Kwa mujibu wa Meneja Mawasiliano David Mziray.
Kauli hii inaufanya umma wa watu ambao sasa ni waelewa kwa asilimia kubwa kuamini kuwa baadhi ya taasisi za serikali watendaji wake wanafanyakazi pasipo kujua wanafanya kazi gani.
Haiwezekani leo hii useme kuwa Boti ile inawezekana iliongeza abiria njiani...sasa wapi kuna gati huko baharini na hao abiria wanatokea wapi? ilhali safari ya boti kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar (Unguja) hakuna kituo hapo njiani.
Lakini labda SUMATRA wana gati mpya Bagamoyo au Mbezi Beach huko. Ila hakika huu ni mtokoto wa mwaka 2012 na ni dharau kwa roho za watu na mali zao kwa mamlaka yenye dhamana ya kusimamiusafiri nchini. Na chini ndio vielelezo vya uwezo wa meli kutoka kwa mmiliki wa kwanza kabla haijauzwa Zanzibar
Name: MV Skagit
Owner: WSDOT
Operator: Washington State Ferries
Port of registry: Seattle, Washington,
United States
Completed: 1989
Identification: Official Number: D949140
Call Sign: WAA6309[1]
General characteristics
Class and type: Skagit passenger ferry
Length: 112 ft (34.1 m)
Beam: 25 ft (7.6 m)
Draft: 8 ft (2.4 m)
Installed power: Total 2,840 hp from 4 diesel engines
Capacity: 250 passengers[2]
1 comment:
Huyu muheshimiwa atakuwa na shahada ya udaktari fani ya mateology na water navigation.
Post a Comment