Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Ali Abdulla Ali akiwa
na Makatibu wake wakitoka nje ya Ukumbi wa Baraza hilo baada ya
kuahirisha kwa siku moja kikao cha baraza la Wawaklilishi jana asubuhi.
Hatua hiyo imekuja kufuatia msiba uliolikumba Taifa baada ya ajali ya
Meli ya M.V Skagit iliyozama karibu na kisiwa cha Chumbe
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na
Wabunge wa Muungano waliofika Zanzibar Kutoa mkono wa pole hapo katika
ukumbi wa Ofisi ya Baraza la Wawakilishi Mbweni kufuatia Ajali ya Meli
ya M.V. Skagit. Ujumbe huo umeongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Mh. Shamsi Vuai Nahodha.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua baadhi
ya majeruhi wa M.V Skagit waliolazwa katika Hospiotali Kuu ya Mnazi
Mmoja wa tatu kushoto ni rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Hassan
Mwinyi
Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Alfonso E. Lenhardt (kati) akiongea jambo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi kufuatia ajali ya Meli ya M.V Skagit.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwafariji
baadhi ya Watalii na wageni waliokuwa wakija Zanzibar kwa Meli ya M.V.
Skagit iliyopata ajali juzi mchana karibu na Kisiwa cha Chumbe. Kushoto ni Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Mh. Hamad Masoud
Hamad.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema akitoa Taafifa ya
uchunguzi wa awali wa Jeshi hilo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi kufuatia ajali ya Meli ya M.V Skagit hapo Ofiosini
Vuga Mjini Zanzibar.Picha na Saleh Masoud Mahmoud – Ofisi ya Makamu wa
Pili wa
No comments:
Post a Comment