ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 7, 2012

Watanzania waishio ughaibuni watakiwa kujiunga na NSSF WESTADI


 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk Ramadhani Dau akipeana mkono na Bernadeta Kaiza ambaye aliyefika katika banda la NSSF kutoa ushuhuda wake pamoja na kuishukuru NSSF kwa kugharamia  safari ya kusafirisha mwili wa marehemu mume wake  (BOFYA HAPA) ambaye alikuwa mwanachama wa NSSF WESTADI aliyefariki  Nchini Marekani na kusafirishwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kutoka Washington, DC mpaka Tanzania kwa ajili ya mazishi.
 Mkuu wa Uhusiano na Hudumna kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume akitoa maelekezo kwa Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi walipotembelea Maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi walipofka katika banda la NSSF katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es salaam.

Mtanzania anayeishi nchini Marekani,  Bi. Bernadetta Kaiza ametoa wito kwa watanzania wanaoishi ughaibuni  kujiunga na mafao ya Welfare Scheme  for Tanzanian Diaspora (NSSF WESTADI) huduma ambayo itamuwezesha mwanachama kupata huduma ya kusafirishwa kutoka nchi husika mpaka nyumbani Tanzania pindi anapofariki.

Akizungumza katika banda la NSSF  mbele ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF) waliofanya ziara katika Maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam alkisema: "Kujiunga NSSF WESTADI kutasaidia mwanachama kugharamiwa safari ya kusafirisha mwili kutoka nchi yoyote mpka Tanzania na kuondokana hali ya kuchangihana fedha pindi mmoja wetu anapofariki."

"Wakati mwingine tunashindwa kusafirisha mwili kutokana na kukosa fedha lakini kwa kupitia huduma hii ya NSSF WESTADI sasa matatizo ya muda mrefu tuliyokuwa nayo sasa yatakwisha endepo watu wengi watajiunga na huduma hii kutokana na gharama zote za mwanachama kugharamiwa na NSSF, aliongeza Bi. Bernadeta Kaiza wakati akiishukuru Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF kwa kufanikisha safari ya kuja Tanzania pamoja na mwili  wa marehemu mume wangu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk Ramadhani Kitwana Dau amesema kuwa  ili kujiunga na mafao hayo mwanachama anatakiwa kutoa ada ya uanachama ambayo ni Dola za Marekani 300 kwa mwaka na fomu zinapatikana katika mtandao wa NSSF.

No comments: