Wakati zoezi la sensa likiendelea vizuri mkoani hapa, inadaiwa kuwa baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu walilala msikitini usiku wa kuamkia siku ya sensa.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa, Abdulaziz Mkindi, alikanusha madai hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana.
“Hakuna Waislamu waliolala kwenye msikiti jana kwa madai ya kukwepa kuhesabiwa,” alisema Mkindi, na kuongeza waliolala ni mlinzi wa msikiti, wageni na wenye ulemavu.
Hata hivyo, Katibu wa Baraza la Waislamu Mkoa wa Arusha, Sheikh Abdulkarim Jonjo, alisema anazo taarifa za waumini wa dini hiyo kulala msikitini hapo, na akawata wakubali kushiriki sensa.
“Sensa ni kwa ajili ya maendeleo ya watu wote, tukubali kushiriki sensa, kama kupingana basi iwe kwa mambo ya msingi,” alisema.
Akifafanua kuhusu mkesha wao, Mkindi alisema uongozi wa msikiti huo, ulipanga kufanya mkesha usiku wa kuamkia jana, lakini waliamua
kuahirisha na mkesha huo sasa utafanyika usiku wa leo.
“Tuliamua kuahirisha mkesha, moja kwa sababu ya kupisha zoezi la sensa. Suala la kuhesabiwa lilishapita, Waislamu tuliongea na Rais na malalamiko yetu yanafanyiwa kazi, sasa suala la kuhesabiwa ni la mtu binafsi,” alisema.
Kuhusu nia ya mkesha wa leo, Mkindi alisema utafanyika kwa lengo la kuiombea nchi amani na matatizo ya mtu mmoja mmoja.
“Waislamu wana swala maalum ambayo wanatakiwa kuamka usiku na kuomba kuhusu jambo fulani na mkiwa wengi anaweza kuwepo muumini mmoja mwema na ikawa sababu ya kukubalika dua yao,” alisema, na kusisitiza kwamba wamepanga kuiombea taifa amani.
Alisema swala hiyo itaanza saa 8: 15 usiku mpaka saa 10: 30 au 10: 45 alfajiri kesho.
Kwa upande wake, Mratibu wa Sensa wa Mkoa wa Arusha, Margreth Martin, alikanusha kuwepo kwa waumini wa dini hiyo kulala msikitini jana kwa madai ya kukwepa sensa.
Kuhusu vifaa, Margreth alisema vipo vya kutosha na vimewahi kuletwa, isipokuwa visibao vya (reflector) kwa makarani hivyo bado havijaletwa.
Hata hivyo, alisema kasoro hiyo haiwezi kuzuia kazi ya sensa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema hadi jana hakuna mtu aliyekuwa akishikiliwa kutokana na vurugu au kugomea kushiriki sensa.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment