Nakala ya barua ya askari Dunga kwa Waziri wa Mambo ya Ndani
Nakala ya barua inaendelea hapa
Danstan Shekidele
Siku chache kabla ya kifo chake askari polisi mwenye namba F 3276, Donald Mathew (33), aliyejinyonga juu ya mti katika daraja la Shani, mkoani Morogoro alimwandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani kueleza kinachodaiwa kuwa ni ufisadi unaofanywa na vigogo wa polisi nchini, imebainika.
Polisi huyo aliyefahamika sana kwa jina la Dunga aliwahi kutoa tuhuma nzito dhidi ya maofisa, wakaguzi na polisi wa kawaida, mkoani Morogoro mwaka jana lakini hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya maofisa hao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fustine Shilogile, jana alisema jeshi hilo, lilipokea taarifa za kujinyonga Mathew jana asubuhi.
Alisema askari huyo, aijinyonga kwa kutumia vipande vya kamba ya kanga ambavyo viliunganishwa na hakuacha ujumbe wowote unaoeleza sababu ya kuchukua uwamuzi huo.
Alisema askari huyo kabla ya kufanya tukio hilo, alionekana mitaani akinywa pombe katika Baa ya Shani.
Alisema baada ya kuonekana amelewa, Mathew aliamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu, kitendo kilichofanya baadhi ya askari polisi waliokuwa eneo hilo, kumfuata na kumsihi avae nguo.
Alisema marehemu, alihamishiwa mkoani Singida kikazi, lakini Novemba, mwaka jana aliamua kuacha jeshi.
“Pamoja na kwamba marehemu aliacha kazi mwaka jana, sisi kama jeshi bado tunamtambua kama askari mwenzetu… kwa msingi huo tutasafirisha mwili wake Agosti 8, mwaka huu kwenda nyumbani kwake mkoani Kilimanjaro,” alisema Kamanda Shilogile.
Alipoulizwa kama kifo cha Mathew kimesababishwa na baadhi ya askari waliohusishwa kwenye tuhuma za kuhusika na biashara za dawa za kulevya, Kamanda Shilogile alisema uchunguzi unaendelea, na kwamba ikibainika kama kuna askari aliyehusika atachukuliwa hatua kali.
Hata hivyo, askari huyo mwishoni mwa mwaka jana, alitoa tuhuma mbalimbali ambazo zilichapishwa katika moja ya magazeti linalotoka mara mbili kwa wiki, zikiwatuhumu askari 9 wa kikosi cha kupambana na majambazi wa kutumia silaha kupokea rushwa kutoka kwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya.
Tuhuma nyingine alizotoa ni polisi kukamata majambazi wenye silaha, lakini huachiwa baada ya kupewa fedha na mali mbalimbali, hivyo kushindwa kuwafikisha kituoni.
Alisema tuhuma nyingine ni polisi kuwakamata wafanyabiashara wa pombe haramu aina ya gongo na bangi bila kuwachukulia hatua zozote baada ya kuhongwa.
Tuhuma nyingine, zinazodaiwa kufanywa na askari hao ni kushirikiana na matapeli, kutapeli raia wa kigeni na kushirikiana na majambazi kuvunja maduka na kuiba mali za wafanyabiashara nyakati za usiku.

Blogzamikoa
6 comments:
Tanzania mafia haya ndo matunda ya CCM. Alafu tutaambiwa inaundwa tume ya uchunguzi .........ndo imetoka.
Huu ni ushahidi mwingine kuwa Tanzania ni nchi ya amani na utulivu.
Tanzania kwa kweli tunakoenda si kuzuri Viongozi mko very selfish kwenye katika Jambo na wala hamuwazi maisha ya watu wengine ambao wako chini masikini kama Mimi! Nina amini haya yote huyu Askari alichokiongea ni cha kweli kuhusu watu (Viongozi) wanavyomis use uongozi wao. Na serikali inajifanya kama vile hawaoni wala hawajui ni kitu gani kinachoendelea, wanaju sana ila they are ignoranto and selfish. And if they are not then why they dont follow laws or Rules and Regulation. Usikute Viongozi mafisadi wame mblack mail huyo Askari hatimae akaamua kujiua Kaka wa watu. Viongozi Maafisadi wanaongoza kwa ufisadi, Uongo, Ulaku na most of it Uchawi!
Kama kweli serikali inataka kweli kuokoa Tanzania kwa nini wasiwape wananchi Haki zao? Na kuwapa uongozi watu wengine. I`m sure kuna watu kibao wamekwenda Shule na Vijana wamesoma Nchi za Nje na wana jua how to act kwenye Laws ! Tanzanian people wake up, ask your self kwanini Serikali hawataki kupitisha Sheria ya kuwa na Uraia Miwili ask your self why? They know that people are so angry and thirsty for new Leaders and Most of these good leaders are young Tanzanian who happened to get a chance to study abroad so they can come to make Different to their country (Tanzania). Most of the young people who got a chance to lead our are the same Leaders` Sons and Daughter and guess what hao watoto wanaact the same thing as wazazi wao walio madarakani, and I hate this. Na ndio maana nchi haiendelei. Tanzania sasa hivi imekuwa kama Dangulo fulani, yaani kama wewe humjui mtu aliye madarakani then no Jobs for you! Okay tell me Serikali after this thing what are you going to do? Singizia uchunguzi, I`m sick of it, ah! We really need change Tanzania! And not for special people but for everyone, Gosh!
This is ridiculous! Nchi yetu imefika mahala pabaya sana
Mh.Waziri wa mambo ya ndani upo wapi! ebu angalia vitendo vichafu vinavyofanywa na askari polisi kwa raia wao?
Mtu atajinyongaje alafu miguu ikajikunja hivyo? Mtu aliyejinyonga miguu inakuwa imekakamaa straight na wala haiwezi kugusa chini. Mbona hata ku-stage kifo wameshindwa? Hii ni laana Tanzania.
Post a Comment