UWT-US
UMOJA WA WANAWAKE
TANZANI-MAREKANI
Kwa furaha
kubwa tunapenda kuwatangazia wanawake wote waishio Marekani kujitokeza kwa
wingi na kujiandikisha uanachama wa UWT MAREKANI. Tawi hili limeanzishwa na
Mwekiti wasasa hivi Mrs Eliserena Kimolo na Mshauri kutoka upande wa akina kaka, Givens Kasyanju.
Malengo na madhumuni ya umoja huu nikumlenga
kila mwanamke wa Kitanzania na wale walio olewa na Wanzania na Watoto waishio
Marekani ( US ), Katika Nyanja mbalimbali zikiwemo;
- Maendeleo
ya Wanawake na Watoto, kiafya, Kielimu
na Kiuchumi.
-
Kudumisha/Kutangaza na kuendeleza Utamaduni wa Mtanzania.
- Haki za
wanawake na watoto. (Vitendo vya
ukatili)
- Amani na
Usalama katika Jamii na Nchi yetu.
- Kuwasaidia
wanawake na Watoto walioko nyumbani Tanzania.
- Biashara –
Kuboresha na kuinua vipaji, biashara kwa
Wanawake na Watoto.
- Na
mengineyo yahusio Familia zetu. (Jamii yetu)
Kwa kifupi
zaidi tuna penda kuwafahamisheni wote kuwa, Umoja huu wa Wanawake hapa Marekani
ni wa kila Mwanamke wa Kitanzania bila
kujali Rangi, Dini, Kabila, Siasa, Wapi umetoka na maumbile ya viungo. Hivyo
basi, tuomba Wanaweke wote kushirikiana pamoja kwa sauti na nguvu moja ya maendeleo
katika Jamii yetu.
Kwa sasa
hivi tumia emails hizi katika kujiandikisha
1 comment:
duh! hizi jumuhiya ni nyingi kichizi.sasa tujiunge wapi???
CCM,CHADEMA,ATC-METRO,UWTamerica,TAMUCO...au kile chama cha wanawake wa DC sijui kinaitwa nini.Mama Kimoro upo katika jumuhiya ya wa Tanzania kwanini hizo nyanja za UTWamerica zisiwe implemented kwenye jumuhiya....
Post a Comment