ANGALIA LIVE NEWS

Friday, September 7, 2012

AFUNGUKA KUHUSU MAPENZI YAKE NA MWANAUME MWENYE UMRI KAMA BABA YAKE


Herieth katika mapose na mpenzi wake aka mume wake
MSANII wa filamu bongo Herieth Amos, amefunguka kuwa kuolewa kwake mwanaume aliyemzidi umri na kuhongwa gari hakumaanishi kuwa amefuata hela pale ni mapenzi aliyonayo.


Msanii huyo anafanya vizuri kwenye tasnia ya filamu, na tayari ameshacheza filamu nyingi, ambazo zimemweka juu na kumtangaza katika tasnia hiyo.

Baada ya kusikia maneno mitaani kuhusiana na ishu hiyo, mtandao wa DarTalk ulimtafuta msanii huyo na alipopatikana alidai kuwa ana mpenzi mume wake na haoni kama maneno ya watu yanaweza kumfanya asinywe maji au kufurahia mahusiano yao. “Kuolewa na mtu mwenye umri mkubwa siyo tatizo kwani mapenzi hayana umri hivyo nachotaka kusema ni kwamba nampenda sana mume wangu na sijali juu ya maneno ya watu ambayo hayana msingi wowote,” alidai Herieth.

Hii ndio gari ya Harieth aliyonunuliwa na mumewe
Alipo ulizwa juu ya kuhongwa gari Herieth alifunguka na kusema kuwa hiyo ni zawadi kutoka kwa mume wake hivyo haoni sababu ya watu kuanza kuzungumzia vibaya ambapo pia anaamini kuwa watu wanaona wivu yeye kuolewa na baba huyo.

Source: DarTalk

No comments: