Mahojiano na Makamu wa kwanza wa Rais ZANZIBAR Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad.
Katika mahojiano haya, Mhe. Hamad anaeleza kile kilichomleta Marekani, hali ya kisiasa Zanzibar
Anajadili maridhiano ya mwaka 2009 na kufafanua ni kwanini alipigania kura za chaguzi za 1995, 200 na 2005 lakini sio 2010 ambapo wengi waliamini ameshinda ukilinganisha na chaguzi zilizopita?
Anazungumziaje dhana ya ukubwa wa serikali Zanzibar ukilinganisha na idadi ya watu wakena ni kwanini tuwe na Makamu wa Kwanza na Makamu wa Pili wa Zanzibar.
Nini kiini cha mgogoro wa sensa?
Na pia, kwa yeye kuwa sehemu ya serikali Zanzibar ilhali ni kiongozi wa chama cha upinzani Bara kunaleta mgongano wa maslahi?
Kwanini CUF inaonekana kupoteza mvuto nchini Tanzania?
Nini anazungumzia kuhusu mgogoro wake na Mhe. Hamad Rashid?
Zanzibar inakabiliana vipi na tatizo la ajira kwa vijana?
Je! Zanzibar ni nchi ya kijamaa ama kibepari?
Vipi anazungumzia tatizo la usafiri nchini Zanzibar?
Elimu je?
Suala la Muungano lina utata gani?
Ni ipi tofauti ya Maalim Seif wa 1995 na huyu wa sasa?
Na mwisho nini wito wake kwa wote wamtazamao sasa?
Ungana nasi
1 comment:
kwakweli wanasiasa wetu matapeli kabisa hawana njia mbadala za kimaendeleo nchini..SEIF kweli anababaisha kujibu mwaswali hivyo ?? mmmhh kweli njaa mbaya..lakini vizuri amekiri mwenyewe lumba linasumbua !!
Post a Comment