ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 27, 2012

CHEKA UNENEPE


Mdada mmoja mke wa mtu alikuwa akisumbuliwa sana na jamaa mmoja aliyekuwa
akimtaka kila siku, hatimae akamwambia mumewe. Mume akamwambia mkewe,
we mkubali tu, ila mwambie aje mlale hapa kwetu, mi ntajificha
uvunguni na panga. Akisha ingia ukiona kamaliza kuvua nguo we
ning’iniza mkono anza kuuchezesha, mi nikiuona mkono nitatoka uvunguni na
kumfunza adabu.
Mdada akafuata masharti ya mumewe na hatimae wakaingia chumbani na
yule bwana, mumewe akiwa tayari na panga uvunguni mwa kitanda. Jamaa alipovua
shati, mke alishangaa kuona ana makovu makubwa kifuani na mgongoni;
MKE: Hee! mbona una makovu hivyo
JAMAA: Niwe mkweli mie nina tatizo sana la kupenda wake za watu, waume wengi wamekuwa wakipanga kunifumania, nimeshafumaniwa mara kumi na
tisa, na wote walionifumania nimewaua.
MKE: He jamani….jamaa akaendelea kuvua nguo alipomaliza mdada akaanza
kuning’iniza mkono ili mumewe atoke uvunguni, mume kabana kimya, kilajitihada za mdada kupunga mkono hazikupata majibu mpaka jamaa kamaliza
shughuli zake akatokomea.
MKE: Jamani sasa ndio nini? Mbona hukutoka
MUME: We we we, mwenyewe umesikia kasha ua 19 unataka niwe wa ishirini

1 comment:

Anonymous said...

yoo hii kali tena hatari na ina asali duuu ebwana eeh
mdau NY