ANGALIA LIVE NEWS

Friday, September 7, 2012

MAJAMBAZI WATATU WAKAMATWA ARUSHA WAKIWA NA SILAHA NA MIHURI YA SEREKALI

 kamanda Sabas akionyesha silaha ,risasi na mihuri ambayo majambazi hao
 wamekuta nazo
Jeshi la polisi mkoani Arusha limefanikiwa kuwakamata majambazi sugu  watatu wakiwa na silaha aina ya pisto yenye risasi tano pamoja na mashine ya kuonyesha bunduki , kifaa cha kubustia risasi pamoja na risasi 46 za bunduki aina ya smg Katika matukio mawili tofauti.

Akiongea na waandishi wa habari mkoani hapa kamanda wa polisi mkoa  wa Arusha Liberatus Sabas alisema kuwa matukio hayo mawili yalitokea  kwa nyakati  tofauti Katika maeneo tofauti ya mkoani hapa kufuatia msako mkali uliokuwa ukifanya na jeshi la polisi pamoja na ushirikiano wa wananchi wasamaria wema.

Alisema kuwa Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni jambazi sugu aliyefahamika kwa jina la Salimu Kiwele alimaarufu kwa jina la Msaula(39)mkazi wa sombetini mkoani hapa akiwa na mke wake  aliyetambulika kwa jina la Princes Juma (34) wote ni wakazi wa sombetini wamekamatwa   nyumbani kwao wakiwa na silaha pamoja na risasi.

Alisema kuwa watu hao walikamatwa wakiwa na silaha aina ya pisto  Glock FFN 350 ikiwa na risasi tano ambazo zilikuwa ndani ya magazine ya silaha hiyo.

Alisema kuwa mtu  huyu pamoja na mke wake walikuwa wanatafutwa na polisi kwa kipindi cha mda mrefu kufuatia kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu  ,mauaji pamoja na  wizi ambao yameshawai kutokea jijini hapa .

Katika tukio lingine kamanda sabas alisema kuwa  mwanamke mmoja ambaye amefahamika kwa jina la Konsolata Tarimo (30)mkazi wa ngaramtoni amekamatwa na jeshi la polisi akiwa na risasi  46 za bunduki aina ya smg  pamoja na vifaa mbalimbali za bunduki hiyo ikiwemo  kifaa cha kusafishia silaha hiyo.

Alibainisha kuwa mwanamke huyo alikutwa nyumbani kwake majira ya saa nane usiku wa kuamkia September 6 wakati askari waliokuwa doria walipofanya msako wa kushutukiza Katika nyumba hiyo mara baada ya kutilia shaka.

Walisema kuwa walipofanya msako huo  walikuta risasi hizo 46 za bunduki hiyo aina ya smg  ,muhuri ambao ulikuwa umeandikwa pande zote mbili huku pande ya kwanza ikiwa imeandikwa District game office simanjiro na upande mungine umeandikwa district game of monduli district,kifaa cha kubusti risasi Katika bunduki hiyo ya smg pamoja na kifaa cha kusafishia silaha hiyo inayotumiwa na risasi hizo.

Aidha alibainisha kuwa silaha ambayo ilikuwa inatumika kwa ajili ya silaha hiyo haijakamatwa bali msako mkali unaendelea ili kukamata silaha hiyo iliyokuwa ikitumia risasi hizo.
chanzo  libeneke la kaskazini 

No comments: