ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 27, 2012

MAREHEMU AGNESS YAMO AAGWA LEO, KUZIKWA MOROGORO KESHO



 Wanahabari, ndugu, jamaa na marafiki wakipita kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa gazeti la Tanzania Daima, Agness Christopher Yamo, na kutoa heshima zao za mwisho, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilizofanyika leo mchana Buguruni, jijini Dar es Salaam, ambapo baada ya kuagwa marehemu alishafirishwa kuelekea mjini Morogoro kwa maziko. 


Yamo alifariki dunia jana katika hospitali ya Jeshi, Lugalo, Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kwa matibabu. Mungu ailaze roho ya marehemu Agness mahala peponi, Amin.

Sehemu ya waandishi wa habari wanawake waliojitokeza katika msiba huo leo.

No comments: