ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, September 16, 2012

SIKU NA USIKU WA MTANZANIA WASHINGTON, DC

Siku ya Mtanzania iliyoanzia Ubalozini Asubuhi na kumalizikia Lanham, Maryland usiku na kuhudhuliwa na Watanzania na marafiki zao kutoka kila kona ya Marekani ilikua ni siku na usiku wa kuhistoria tunatoa shukrani kwa Balozi na Ubalozi wetu Washington, DC kwa kuanzisha siku hii naVOA kufanya Matangazo yao ya moja kwa moja toka Ubalozini hapo.
Watu wengi walipendekeza siku hiyo ya Mtanzania ifanyike kila mwaka wakati wa Labor Day Weekend ili kutoa fulsa kwa Watanzania walio mbali kuweza kujipanga na kuhudhulia kwa wingi kwani wiki ya Labor Day Jumatatu hua ni mapumziko.

 Kali TV nao walikuwepo kupata matukia mawili matatu na kuongea na watu mbali mbali kuhusu siku hii ya Mtanzania

Siku ya Matanzania ilijumuisha vikundi mbali mbali kutoka Marekani na Tanzania, kundi lililowavutia wengi ilikua kundi la ngoma za asili kutoka New York lilikua likiongozwa na Mtanzania Erick Fungo akiwa na wenzake wenye asili ya Marekani waliocheza ngoma za asili za Tanzania kwa Ustadi mkubwa, kikundi kingine kilichawavutiwa Watu ni kundi la wacheza showa wa Diamond ambao nao waliipanda siku hii ya Mtanzania show kabambe iliyowafanya Watanzania na marafiki zao kushindwa kujizuia kukaa chini muda wote.
Sehemu nyingine ni Hafsa Kazinje mwanamuziki aliyeiimba wimbo wa Presure akimshirikisha Banana Zolo alitikisa jukwaa kwa staili za pakee pale Mhe. Balozi na Watanzania wengine walipojiunga nae kucheza pamoja yote ni kuipamba siku ya Mtanzania mbali na Wajasiliamali waliokuwepo na maonyesho ya vitu vyao au shughuli wazifanyazo kuitangaza Tanzania bila kuwa sahau wapishi wa DMV waliojumuika pamoja na Watanzania wenzao kwa vyakula vya kila aina.

Kitu kingine kilichokua kivutio ni Watanzania waliojitokeza wamevaa kiasili kulikopelekea watu kutaka kufanyike mashindano ya mavazi ya asili mwakani
Watu wengi walikuja na familia zao kwenye siku hii ya Mtanzania na kufanya watoto wengi kukutana na watoto wenzao na kujifunza mambo mapya ambayo walikua hawjui kuhusu Tanzania
Siku iliishia Lnham, Maryland kwa Watanzania kucheza Rhumba na pia vikundi mbali mbali zikiwemo Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi kutunukiwa vyeti kwa kuwezesha kwa njia moja au nyingine kufanikisha siku hii ya Mtanzania.

No comments: