Msafara
maarufu duniani unaohusisha wanyama aina ya Nyumbu umeanza kurejea
katika makazi yao ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakitokea mapumziko
katika nchi ya jirani.
wageni wakiwaelezeawaandishi wa habari jinsi safari yao ilivyokuwa
mwenzangu uyu maji yalimzidi
Kila
mwaka, nyumbu pamoja na wanyama wengine kama pundamilia na swala
hufanya mzunguko maalum unaochukua miezi 12 ya mwaka ambapo miezi kumi
kati ya hiyo huwepo nchini katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na
iliyobaki hutumiwa na wanyama hao katika eneo la Hifadhi ya Masai Mara
nchini Kenya.
Mwaka
huu msafara huu unaohusisha wanyama zaidi ya Milioni Moja na Nusu na
ambao hutembea katika mzunguko wa takribani Kilometa 1,000 umewahi sana
kurejea nchini ukitokea mapumziko nah ii kwa mujibu wa taarifa za
kitaalamu inatokana na kuwahi kunyesha kwa mvua katika eneo la Serengeti
ambapo imesababisha kuwepo na nyasi nzuri ambazo ni chakula muhimu kwa
wanayama hawa.
Changamoto
kubwa wanayokutana nayo msafara huu mara unaporejea nyumbani ni tukio
la kuvuka Mto Mara ambao umejaa wanyama wakali aina ya mamba na viboko
ambao nao huwa ni msimu wao wa kujipatia chakula kwa kuvizia na hatimaye
kuwakamata wanyama hawa mara wanapovuka mto.
Watalii
kutoka maeneo mbalimbali duniani wamekuwa wakifurika katika Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti kushuhudia tukio hili adimu la kuvuka Mto Mara ambalo
wengi wao wamekuwa wakiliona kupitia filamu mbalimbali zilizotengenezwa
katika eneo hili.
No comments:
Post a Comment