Jeshi nchini Nigeria linasema kuwa limemuua mtu anayeshukiwa kuwa msemaji wa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram.
Kwa
mujibu wa jeshi hilo, wanachama wengine wakuu wa kundi hilo pia
walikamatwa katika msako mkali wa jeshi uliofanywa ,mapema leo Kaskazii
mwa mji wa jimbo la Kano.Kundi hilo la Boko Haram bado halijatoa kauli yoyote kuhusiana na mauaji hayo yanayodaiwa kufanywa na jeshi.
Mamia ya watu wameuawa mwaka huu pekee katika mashambulizi yaliyofanywa na Boko Haram, Kaskazini mwa Nigeria.
Inaarifiwa
kuwa jeshi lilisimamisha gari lililokuwa linashukiwa kumbeba mwanachama
mkuu wa kundi hilo pamoja na maafisa wengine wakuu wa kundi hilo.
Duru
zinasema kuwa mmoja wa washukiwa waliokuwa ndani ya gari hilo alijaribu
kutoroka lakini polisi waliweza kumpiga risasi na kumuua.
Baadhi
ya watu waliokuwa ndani ya gari hilo wameambia polisi kuwa mtu
aliyeuawa ni msemaji wa kundi la Boko Haram ambaye pia alikuwa anatumia
jina bandia la Abul Qaqa.Jeshi la polisi linasema linafanya kila hali
kuhakikisha linamtambua mtu huyo.
Chanzo: http://www.bbc.co.uk/swahili/habari
No comments:
Post a Comment