ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 19, 2012

HIVI NDIVYO VIKOSI VYA USALAMA VILIVYO DHIBITI HALI YA VURUGU DAR ES SALAAM LEO


Barabara ya kuingia katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi zikiwa zimefungwa na Askari Polisi kufuatia vurugu zilizotokea leo
Polisi wakifanya doria kwa kutumia pikipiki
 Mitaa ya Kariakoo na viunga vyake ikiwa imeimarishwa na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika mitaa ya Kariakoo leo
 Ulinzi uliimarishwa na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika mitaa ya Kariakoo leo
 Wanajeshi wakivinjari katika mitaa ya Kariakoo leo
 Askari wa jiji wakishiriki kikamilifu katika zoezi la kuwakamata watu waliokuwa wamekusanyika kwa nia ya kutaka kuandamana katika eneo la Kariakoo
Magari ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa katika doria katika barabara ya Msimbazi ambako kulitokea vurugu zilizosababishwa na waislamu waliotaka kuandamana.
Watu hao walifika mmoja mmoja maeneo ya Ikulu kabla ya kudhibitiwa na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na kupelekwa Kituo Kikuu cha Kati. Kukamatwa kwa watu hao kunafuatia Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwatawanya waumini wa dini ya Kiislamu ambao walikuwa na nia ya kufanya maandamano.
Waandishi wameshuhudia gari mbili za jeshi la Polisi zikiwa zimebeba wanajeshi waliokuwa na silaha. Katika maeneo ya Kariakoo vikosi vya Jeshi la wananchi wa Tanzania vimekuwa vikifanya doria ili kuimarisha hali ya ulinzi.

Picha zote kwa hisani ya Michuzi Blog

No comments: