James Magai
MWALIMU wa Shule ya Msingi Wabegi iliyoko Bunju Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Janeth Tijani Mahunguhungu (50), amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela, baada ya kupatikana na hatia ya kughushi wosia wa marehemu.
MWALIMU wa Shule ya Msingi Wabegi iliyoko Bunju Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Janeth Tijani Mahunguhungu (50), amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela, baada ya kupatikana na hatia ya kughushi wosia wa marehemu.
Mwalimu huyo alihukumiwa adhabu hiyo na Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, baada ya kumtia hatiani kwa mashtaka yote mawili yaliyokuwa yakimkabili.
Katika shtaka la kwanza, mshtakiwa huyo alikuwa akidaiwa kughushi wosia wa Marehemu Tijani Mzee Mahunguhungu, na katika kosa la pili alikuwa akidaiwa kuwasilisha mahakamani wosia huo wa kughushi, ili ateuliwe kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu.
Wosia huo unaoonesha kuwa umetolewa na kusainiwa na marehemu Mahunguhungu April 25, 2003, unaeleza kuwa mshtakiwa ndiye mrithi wa mali zote za marehemu na kwamba watoto wote wa marehemu (wa mke mkubwa wa marehemu) hawana nafasi ya katika mirathi hiyo.
Katika hukumu yake iliyosomwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Athman Nyamlani kwa niaba yake, Hakimu Mkazi Othman Kasailo aliyekuwa akisiliza kesi hiyo alisema kuwa ameridhika kuwa upande wa mashtaka umethibitisha mashtaka hayo.
“Mahakama hii inaona kuwa upande wa mashtaka umethibitisha mashtaka, na inamtia hatiani mshtakiwa kwa makosa yote mawili,” alisema Hakimu Kasailo katika hukumu hiyo.
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote Hakimu Nyamlani kwa niaba ya Hakimu Kasailo alisema: “Hivyo katika kosa la kwanza mshtakiwa atafungwa jela miaka mitano na katika kosa la pili pia atafungwa jela miaka mitano. Adhabu zote hizo zinakwenda kwa pamoja.”
Katika hukumu hiyo, Hakimu Kasailo alisema kuwa katika kosa la kwanza, anaridhika na ushahidi wa shahidi wa kwanza na wa tatu ambao ni watoto wa marehemu Mahunguhungu, ulioungwa mkono na shahidi wa pili [Mtaalamu wa maandishi] na shahidi wa tano.
Alisema kuwa kwa kuwa shahidi wa kwanza na wa pili ni watoto wa marehemu, ni wazi kuwa walikuwa wakiujua mwandiko na saini ya marehemu baba yao, kama walivyoieleza mahakama.
“Kwa kuwa wana mazoea na mwandiko na saini ya baba yao, mahakama haina shaka kwamba ushahidi wao ni wa kweli, kama walivyoieleza mahakama kwamba mwandiko na saini iliyokuwa ikibishaniwa si vya marehemu, bali ni vya kughushi,” alisema.
Alifafanua kuwa kwa mujibu wa sheria ya ushahidi, maoni ya mtu mwenye uzoefu wa mwandiko unaobishaniwa ni bora hata kuliko maoni ya mtaalamu wa maandishi.
“Kwa kuwa PW1 na PW3 wote walikuwa na mazoea ya mwandiko na saini ya marehemu, ni dhahiri kuwa ushahidi wao ni wa kuaminika. Hivyo Mahakama inaamini mwandiko na saini ya marehemu Mahunguhungu ilighushiwa,” alisisitiza.
Kuhusu kosa la pili, Hakimu Kasailo alisema kuwa lilithibitishwa na PW4, aliyeieleza mahakama kuwa mshtakiwa alikwenda kuapa mbele yake, kama Kamishna wa viapo, katika Mahakama ya Mwanzo Manzese, akiwa na wosia huo.
Aliongeza kuwa hata shahidi wa sita (mplelezi wa kesi), aliieleza mahakama kuwa alimkamata mshtakiwa na kumhoji, akakiri kuwasilisha wosia huo mahakamani, lakini akakana kuwa si wa kughushi.
Aliongeza kuwa hata shahidi wa sita (mplelezi wa kesi), aliieleza mahakama kuwa alimkamata mshtakiwa na kumhoji, akakiri kuwasilisha wosia huo mahakamani, lakini akakana kuwa si wa kughushi.
Baada ya kumtia hatiani, Mwendesha Mashtaka Mutani Magoma aliiomba mahakama impe adhabu kali mshtakiwa kwa mujibu wa sharia, ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia za kughushi nyaraka ili kujinufaisha au kukidhi haja za kutenda uhalifu.
Magoma alisema kuwa uhalifu huo umekuwa ukiongezeka hususan jijini Dar es Salaam, na kusababisha dhuluma na kuwanyima watu wengine haki zao.
Hata hivyo Wakili wa mshtakiwa, Majura Magafu, alidai kuwa mashtaka dhidi ya mshtakiwa yalitokana na ugomvi wa mali baina ya walalamikaji na mshatakiwa, kwa kuwa mstakiwa alikuwa ni mke wa marehemu [mdogo]
Mwananchi
No comments:
Post a Comment