Yanga yashinda katika dimba la Sheikh Amir Abeid yailaza Jkt Aljoro 1 kwa 0 goli la wana jangwahao liliwekwa kimiani na Twinte katika dk ya 53. |
Emmanuel Okwi
Timu ya Soka ya Simba yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam leo imezidi kujichimbia kileleni baada ya kubugiza bila huruma timu ya Azam magoli 3-1, katika mchezo wa Ligi kuu Soka Tanzania bara uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa.
Mchezaji Emmanuel Okwi wa Simba leo ameng’ara katika mchezo dhidi ya Azam baada ya kuifungia timu yake magoli 2 huku Mzambia Felix Sunzu akipachika goli la kusawazisha.
Mbali na kichapo hicho Azam ambayo kama Simba ilikuwa inashikilia rekodi ya kutopoteza mchezo hata mmoja tangu ligi ianze, lakini leo imevunjiwa mwiko wake huo na kupoteza mchezo na kushuka nafasi moja kutoka yapili hadi ya tatu.
Yanga iliyokuwa inakipiga na JKT Oljoro mjini Arusha imepanda kwa mara ya kwanza hadi nafasi ya pili tangu ligi hii ianze baada ya kufikisha pointi 20, huku watani wao wa jadi Simba wakiwa mbele kwa Point 2 na Azam ikibaki na pointi 19.
Simba ndio imekuwa timu pekee hadi sasa mabayo haijapoteza mchezo hata mmoja huku ikiwa imetoka sare mara 4 na kushinda michezo 6.
No comments:
Post a Comment