ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 22, 2012

KIONGOZI WA KUNDI LA UAMSHO SHEIKH FARID NA BAADHI YA WAFUASI WAKE WAFIKISHWA MAHAKAMANI LEO


Gari la Polisi la pili ambalo liliwachukuwa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO ambao walishitakiwa kwa makosa ya kufanya fujo na uchochezi likiwa linasindikizwa na magari ya Polisi kuja Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe.
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wakiwa wanaimarisha usalama katika eneo la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe ambapo Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO walipelekwa kwenda kusomewa mashitaka yao.
Mmoja kati ya Viongozi wa UAMSHO Shekh Azan Khalid Hamdan (43) akishuka kwenye gari la Polisi kuelekea Mahakamani Mwanakwerekwe kwenda kusomewa mashtaka yao.
Kiongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Shekh Farid Hadi Ahmed akishuka kwenye gari la Polisi kuelekea Mahakama ya Mwanakwerekwe kwenda kusomewa mashtaka yao yanayomkabili ikiwemo kusababisha fujo na uchochezi.
Baadhi ya Wananchi walioenda Mahakamani hapo kwenda kushuhudia kesi inayowakabili Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO ambao walikosa dhamana na kurudishwa Rumande.
Gari la Polisi ambalo liliwachukuwa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO ambao walishitakiwa kwa makosa ya kufanya fujo na uchochezi likiwa linawasili Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe.Viongozi hao wote walirudishwa rumande.

(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

1 comment:

Anonymous said...

Wadau mbona jengo la mahakama halipo pichani? Kama kuna mtu ameliona naomba anisaidie maana sijui kama safari ya kuelekea mahakamani bado inendelea au ndo wameshafika.