Advertisements

Friday, October 19, 2012

NINI SULUHISHO YA HAYA YANAYOENDELEA TANZANIA YETU, NA NINANI WA KUNYOOSHEWA KIDOLE?. MUNGU IBARIKI TANZANIA

Askari Kanzu akimsindikiza kwa teke mmoja kati ya watuhumiwa waliokamatwa wakati wa operesheni maalum iliyowekwa katika jiji la Dar es Salaam,leo mchana ili kuwadhibiti baadhi ya waliodaiwa kuwa ni waumini wa dini ya kiislam, waliokuwa wamepanga kufanya maandano mchana wa leo baada ya Swala ya Ijumaa kuelekea Ikulu kwa lengo la kushinikiza kiongozi wao, Katibu wa Jumuiya za Taasisi za Kiislam, Sheikh Ponda, aliyekamatwa majuzi,aachiwe. Hata hivyo jitihada za watu hao ziligonga ukuta baada ya wao kujipanga kutokea kila kona na kukutana maeneo ya Ikulu, lakini la Askari pia walijiandaa na kujipanga vyema kila kona ya jiji na kuwadhibiti watu hao. 
Vurugu kubwa ilikuwa katika maeneo ya Kariakoo ambako pia walijitokeza baadhi ya vijana waliojichanganya na makundi hayo na kuanza kuvamia maduka na kupora mali za watu na kuwatishia wenye maduka, jambo ambalo liliwafanya Polisi kuwatawanya kwa kupiga risasi hewani na waliokaidi amri hiyo walianza kushughulikiwa kama picha hizi zinavyoonyesha Pata Mkanda Kamili.
Twende garini.....
Akaaaa sio mimi jamaniiiiiii, Babu (kulia} akijitetea...
Askari wakimdhibiti babu...
Babu akishuhshwa garini kuingizwa kituoni.....
Mgambo wa kike akipambana na kijana kumburuta kumpeleka garini, baadaye mgambo huyu CHALIII
Mgambo chaliii, lakini wapi anaye tuuuu....
Watuhumiwa wakipandishwa garini....
Watuhumiwa wakipandishwa garini....
Watuhumiwa wakipandishwa garini....
Jamaa akijaribu kueskep ambapo alikula bonge la mtama na kutambaa kama hivi na kudakwa na mgambo wa kike....

3 comments:

Anonymous said...

Use of exessive force never works and the Police or Army oughts to learn moderation. I hope your politicians and Army generals understands this that may backfire and reach a point of no return which will be sad. i see in this picture like excitation of Army corps enjoying to arrest snd beat for no sensible reason,

Anonymous said...

It looks like excessive force and aggression not sensible with excessive force

Anonymous said...

Jee Watanzania chakujiuliza hii ikuli ni kwa ajili ya Kanisa Katoliki tu?, au waimbe wao Maskofu lakini Akilia Bundi huambiwa Uchuro?.