ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 22, 2012

Msikilize Naibu Waziri wa Elimu wa Tanzania Akitoa Mada Afrika Kusini


11 comments:

Anonymous said...

Matakeo ya elimu ya upe, mawaziri wetu kizungu kinasumbua, je tutafika?

Anonymous said...

I did not know if there is an island of Zimbabwe in Tanzania.

Anonymous said...

Poor english, poor knowledge, poor everything. poor poor...poor. That is our minister for EDUCATION? Tutabaki hapo hapo! Madudu madudu! Hata mtu mwenye dementia angekumbuka nchi yake haina sehemu inaitwa Zimbabwe! Kikwete yupo wapi? Hao ndio mawaziri aliowachagua na bado anaona ni wasomi na ana timu imara! HONGERA KWA KUTUFAHAMISHA KUWA ZIMBABWE NI SEHEMU YA TANZANIA!! ASANTE SANA MHESHIMIWA WAZIRI.

Anonymous said...

AMEBORONGA KILA KITU. ANGALIA SASA ANATUKOSANISHA NA ZIMBABWE. TUTAANZA KUWEKEWA VIKWAZO SASA NA NCHI ZA MAGHARIBI KWA SABABU YA HUYU MUGABE. NADHANI HUYO MZUNGU ANAYEMWANGALIA HAPO ANAMUONEA HURUMA. HUYU NAIBU WAZIRI NI MMOJA KATI YA MAMIA YA VIONGOZI WANAOPIGANA VIKUMBO KUWANIA PER DIEM. UTASIKIA WAKISEMA MHESHIMIWA AMETUWAKILISHA VIZURI SANA.

Unknown said...

Its amaizing how our country is well vested with brilliant leaders, they trully know the boundaries of our country. Be blessed my loved country.

Anonymous said...

Kwa hii! Nafikiri Mh. Mkuu sana amepata jibu la kwa nini mawaziri wasiwe na elimu na ujuzi vinavyohusiana na wizara wanazoziongoza. Yale majibu mepesi ya eti kwamba Uwaziri hausomewi, ndiyo athali yake hii. Hivi ulimwengu unatufikiriaje sisi watanzania kama muwakilishi wetu wa wizara tena ya ELIMU ndo anawasilisha mada kwa namna hiyo? Je, sisi wengine tungewasilisha vipi???
Tafakari!!!

Anonymous said...

Tatizo hapa siyo kizungu tu! Nionavyo mimi, hata ule ufahamu tu wa jiografia ya nchi yetu viongozi wetu kama waziri huyu hawana!!! Tangu lini Tanzania imeungana na Zimbabwe? Ni nani amesema Indian Ocean ni nchi ambayo imepakana na Tanzania? Huu mwaka wa 11964 nao ni balaa tupu!! Kibo!! huyu jamaa ndo kachemshaaa kweeeeeli!

Anonymous said...

Je,! Je! Akipewa mkataba mzito wa kiingereza wenye kila la kutumaliza WaTZ atasoma kweli au ndio kusaini tu.
Anasoma kitu tofauti na kilichoandikwa, kwenye hizo power point slides, ukiangalia kwa ukaribu utaona neno Zanzibar, pia 1964. Hata kama hakujiandaa hiyo iko katika historia, na jiografia pia, tena kama yeye ni naibu waziri!!!!Pia kutoa mada (presentation) kwa kusoma mstari kwa mstari sijui kama bado ipo tena, inaonyesha hujui unachokizungumzia, au unasoma hotuba kwa niaba ya mtu mwingine au umeandaliwa na mtu mwingine,(je kusoma ni shida?..Ok kiingrereza ni kigumu kwake ...tuma mwakilishi,au ongea kiswahili utafsiriwe.

Anonymous said...

hivi huyu ni naibu waziri kweli, for this case anatakiwa aondoke mwenyewe maana hata pronunciation yake inaonyesha hana elimu tosha kuongoza " WIZARA YA ELIMU"

Anonymous said...

huwa najiuliza hawana hata muda wa kusoma speech zao kabla ya kufanya presentation,inasikitisha sana maana amesoma ambacho hakipo kwenye speech, kuna mambo mawili kwa waziri huyo kwanza lugha hiyo (English), imekuwa ni lugha ngumu mdomoni mwakwe hasa katika kuitamka kilichoandikwa, jambo la pili speech nayo ilikuwa haijakaa vizuri, na uwoga ulikuwa umemtawala, swali ninalojiuliza waziri wetu ni kayumba sasa viongozi wa wizara na wanafunzi watakuwaje? namshukuru mungu maana madhara yanaanza kuonekana kutokana na elimu yetu hapa nchini ilivyo duni kuna haja ya kuanza kuangalia tena ubora wa elimu yetu kutokana na alama za nyakati na dalili tunazoziona!.

Anonymous said...

Huyu jamaa alikuwa busy anafanya shopping ya suti za kuja kuvaa bungeni. Hakupata muda wa kupitia presentation yake-aliyoandaliwa. Lakini kwanini aandaliwe speech? Kazi yake ni nini? Aibu sana hii. Sijui alitolewa wapi huyu. Wameachwa watu wenye elimu na kupewa yeye kazi hiyo?
Ama kweli matunda ya upe na voda faster tunayaona sasa. Sijui litakuja jina lipi tena after 2015. Hongera Kikwete kwa kutuchagulia mwakilishi bomu!!