TUNAAMBIWA kuwa kuishi vizuri ni pamoja na kula chakula bora na sahihi. Pia, mtu anayeishi vizuri ni yule ambaye hasumbuliwi na maradhi hatari na njia pekee ya kuulinda mwili dhidi ya maradhi hatari ni kujua ipasavyo na kuvitumia vyakula bora pamoja na kufanya mazoezi.
Katika makala yafuatayo, nitakuorodhoshea baadhi ya vyakula vinavyotajwa kuwa bora (super foods) ambavyo faida zake mwilini vimeanishwa. Kwa mlaji, linakuwa jambo la busara kujua faida ya kila chakula unachoingiza tumboni. Kwa mujibu wa mwandishi wa makala kuhusu vyakula hivi bora, Bw.Hakeem Rahman, hivi ni vyakula vinavyowafanya “wenye afya nzuri kuendelea kuwa na afya nzuri zaidi na wenye afya mbovu, kuwa na afya nzuri.”
Katika makala yafuatayo, nitakuorodhoshea baadhi ya vyakula vinavyotajwa kuwa bora (super foods) ambavyo faida zake mwilini vimeanishwa. Kwa mlaji, linakuwa jambo la busara kujua faida ya kila chakula unachoingiza tumboni. Kwa mujibu wa mwandishi wa makala kuhusu vyakula hivi bora, Bw.Hakeem Rahman, hivi ni vyakula vinavyowafanya “wenye afya nzuri kuendelea kuwa na afya nzuri zaidi na wenye afya mbovu, kuwa na afya nzuri.”
SAMAKI
Wana virutubisho aina ya Omega 3 ambavyo huulinda moyo dhidi ya maradhi. Samaki pia wana virutubisho vinavyomuongezea mlaji uwezo wa kukumbuka (memory), kuna virutubisho vyenye uwezo wa kupambana na kansa mwilini, kuongeza kinga mwilini na kuondoa mafuta mabaya mwilini (Bad cholesterol). (unashauriwa kula samaki kwa wingi kadiri uwezavyo).
Baadhi ya virutubisho muhimu vinavyopatikana kwenye samaki ni pamoja na vitamini D, vitamin 12, vitamini B3, vitamini B6, Omega 3 Fatty acids, protini na madini mengine mengi.
KARANGA
Unaweza ukazidharau karanga, lakini zina faida kubwa mwilini. Miongoni mwa faida zake ni pamoja na kuimarisha afya ya moyo, hupunguza kolestro mbaya mwilini na kuongeza kolestro nzuri. Mafuta mazuri yaliyomo kwenye karanga hupunguza shinikizo la juu la damu na huponya magonjwa ya moyo na hupunguza uzito. Faida zote hizi unaweza kuzipata kutoka kwenye karanga au siagi iliyotengenezwa kutokana na karanga (peanut butter). (unashauriwa kula kiasi kadhaa kila siku, hasa za kuchemsha ndiyo nzuri).
KAROTI
Miongoni mwa faida nyingi za karoti ni pamoja na kushusha kolestro mbaya mwilini, kupunguza unene, kuimarisha nuru ya macho, kuimarisha shinikizo la damu, inatoa kinga kwenye figo na inaimarisha sukari mwilini. (kula kadiri unavyoweza, mbichi au zilizochemshwa).
MAHARAGE YA SOYA
Haya ni maharage bora kabisa ambayo yana faida nyingi mwilini, ikiwemo kushusha shinikizo la damu, kuimarisha sukari mwilini, kupambana na ugonjwa wa kisukari, figo, moyo, kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa kansa ya kibofu na magonjwa mengine ya wanawake.
PAPAI, TIKITI MAJI
Miongoni mwa matunda muhimu mwilini ambayo hata mgonjwa wa kisukari anashauriwa kuyala ni pamoja na papai na tikitimaji ambayo yanaelezwa kuwa na kiwango kikubwa cha ufumwele (fibre) na hivyo kutoa mchango mkubwa sana katika kuimarisha kiwango cha sukari mwilini. (kula kiasi cha moja katika ya matunda hayo mawili, kila siku).
KITUNGUU SAUMU
Hiki ni kiungo cha mboga, licha ya kuonekana kama ni kiungo cha kuongezea ladha tu ya chakula, lakini ni miongoni mwa vyakula vyenye faida kubwa katika afya zetu. Kitunguu saumu husaidia kuyeyusha damu mwilini hivyo kumuepusha mlaji kushikwa na ugonjwa wa moyo pamoja na presha. Kitunguu hicho pia hutoa kinga kwenye ini na huondoa maumivu ya viungo. Kula angalau kitunguu kimoja mara moja kwa wiki.
GPL
4 comments:
shukran mkuu kwa kutuwekea hii kitu ni fresh sana ila tufafanuliye mmana ya cholesterol ni nini because katika jamiii yetu neno hili si wote wanalijua na kulifahamu vizuri
kwa nini yawe maharagwe ya soya yasiwe maharagwe ya kawaida,hii ni kuuza biashara za watu bwana tanzania huwa hatuyapendagi maharagwe haya labda huko kwenu majuu mkuu luke
si mmeona wenyewe sasa kula samaki ni deal ndo maana sisi watu wa visiwani mungu katubariki kwa hilo kula nyama nyama kwanza kunakufanya moyo wako uwe mgumu na ukatili ndo maana watu wa visiwani wako poa na ruksa na mnawafanya wapuuzi
Nakushukuru sana mkuu kwa kuweka maada hii adhim na kutuelimisha shukran sana bwana mdogo, ninachotaka kussema ni hichi hii cancer ni biashara mkuu wameshagundua dawa ya kutibu cancer na ukimwi lakini hawataki kutoa bure bure hata siku mmoja amin usi amin.
na mungu mkubwa kwa kutulinda kila siku ndo maana unatakiwa umshukuru unapo kula chakula chako na baada ya kumaliza ni yeye peke anaye na atakaye tulinda kwa maradhi yote haya ni vizuri kujilinda lakini kama nguvu zake na baraka za muumba wako hazipo unadhani atakulinda nani hebu jaribu kutafakari hili ukiwa na mudaa
shukran tena bwana mdogo kwa maada hii adhim
Post a Comment