ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 15, 2012

WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR WATOA MAONI KUHUSU KATIBA MPYA

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (aliyesimama) akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (hawapo pichani) wakati wa mkutano uliotishwa na Tume hiyo jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012 katika Ukumbi wa Mikutano wa Baraza hilo mjini Zanzibar, uliolenga kukusanya maoni ya Wajumbe hao kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba. Kutoka kulia ni Wajumbe wa Tume hiyo, Profesa Paramagamba Kabudi, Suleiman Ali, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ali Abdalla Ali, Mjumbe wa Tume Joseph Butiku, Katibu wa Tume Assaa Rashid na Naibu Katibu Casmir Kyuki.

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia kwa makini mkutano wa kukusanya maoni kuhusu Katiba Mpya uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, uliofanyika jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012 katika ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo mjini Zanzibar , ambapo wajumbe hao walipata fursa ya kutoa maoni yao kwa Tume hiyo kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.

Mwakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja Zanzibar ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha , akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012, uliolenga kukusanya maoni ya Wajumbe wa Baraza hilo kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.

Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Asha Bakari Makame akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012, ambao ulilenga kukusanya maoni ya Wajumbe hao kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya.

Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Mhe. Said Ali Mbarouk, akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012, ambao ulilenga kukusanya maoni ya Wajumbe hao kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya.
Kwa picha zaidi Bofya read more

Mhe. Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (hawapo pichani) wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012, ambao ulilenga kukusanya maoni ya wajumbe hao kuhusu Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba na Mjumbe wa Tume Joseph Butiku.

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia) akiongozwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho (kushoto), kuwaaga wajumbe wa Baraza hilo mara baada ya kumalizika kwa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo mjini Zanzibar jana jumapili tarehe 14. Otoba, 2012, ambao ulilenga kukusanya maoni ya Wajumbe hao kuhusu Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.

Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Mhe. Ismail Jussa Ladhu akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012, ambao ulilenga kukusanya maoni ya Wajumbe hao kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya. (FULL SHANGWE)

1 comment:

Anonymous said...

hii yote danganya toto hatutaki katiba mpya wala muungano wa mkataba tunacho taka zanzibar yetu huru yenye mamlala kamili tuwe tunafunga na kufanya biashara zetu huru bila ya kuingiliwa na tanganyika hili si koloni lenu,kuna siku mtang'oka inshallah.

amkeni wazanzibari msiwe mabwege bwana wanakuleteni kila design ya mchakato wa katiba na hakuna hata mmoja walilolifanya kurekebisha kero za muungano.

tugawe ubao kila mtu achukwe ubao wake.tumeshachoka tunataka kupumua tuacheni tupumuwe.

mlipo ungani tulikuwa nchi sasa mmeifisidi mnasema mkoa na kama mliona hakuna maslahi yeyote kwa nini mliungana ni sisi.

msiwe mabegwe wazanzibari hawa watu wameshazoea kutufanya wajinga na wapuuzi wabiyeni wazi hatutaki muungano period/fullstop.

kama hodari warioba mbona kwao ubunge umemshindwa kule bunda na mbona ile tume ya rushwa mpaka hivi leo hajulikana ilipo yayuka.

wanakufanyeni wajinga kila siku nyinyi wazanzibari kwa nini hasa kwa kipi come on man.

wabiyieni hatutaki muungano na wakupigeni mabomu mpaka mfee wote lakini msikubali kuiuza nchi yenu kirahisi rahisi