Mhe. Abdulrahaman Kinana - Katibu Mkuu,
Mhe. Vuai Ali Vuai. Naibu - Katibu Mkuu Zanzibar
Ndugu Lameck Madelu Nchemba - Naibu Katibu Mkuu Bara,
Nape Nnauye - Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi
Mh. Asha-rose Migiro - Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa.
Ndugu Mohamed Seif Khatibu - Katibu Oganaizesheni
Mh. Zakhia A. Meghji - Katibu wa Uchumi na Fedha,
Mwenyekiti wa Chama kwa mujibu wa Kanuni na Katiba ya Chama Cha Mapinduzi, anayo fursa ya kuteua wajumbe kumi (10) wa Halmashauri kuu ya Taifa, ambapo Mwenyekiti aliwateua wajumbe wanne(4) na akabakiza nafasi nyingine sita (6) miongoni mwa wajumbe hao ni Mhe. Asha-rose Migiro, Mhe. Zakhia Meghji, Mhe. Nape nnauye na Mhe. Abdulrahaman Kinana .
Baada ya uteuzi huo Mwenyekiti pia alipendekeza majina ya Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa, ambapo alipendekeza majina yafuatayo;
Nafasi ya Katibu Mkuu, alimpendekeza Mhe. Abdulrahaman kinana.
Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Mhe. Vuai Ali Vuai.
Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe. Lameck Madelu Nchemba.
Nafasi ya Katibu wa Oganaizesheni, Ndugu Mohamed Seif Khatibu.
Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Asha-rose Migiro.
Katibu wa Uchumi na Fedha, Zakhia A. Meghji.
Baada ya mapendekezo hayo, Halmashauri Kuu ya Taifa ilipitisha majina hayo na kuyakubali kuwa hao waliopendekezwa ndio hasa wanaofaa kuwa wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
Pia, Mwenyekiti akawashukuru wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa waliopita na pia kuwataka wajumbe wapya kuchapa kazi, na kuwataka kujenga mustakabali wa Chama, Uimara na Umadhubuti kwa kufanya kazi kwa kushirikiana na kusaidiana.
2 comments:
Jamani huyu kinana si alisema anang'atuka kazi za chama na kuwaachia vijana waingie??? Kulikoni????
this is too much mbegu zilezile na wananchi mnategemea mabadiliko au maendeleo
Post a Comment