TANESCO yaibuka mshindi katika mzunguko wa kwanza
Na: Waaandishi wetu ,
Shirika la Ugavi wa Umeme nchini Tanzania (TANESCO)
limeibuka mshindi wa jumla wa kero kwa wateja wa huduma mbalimbali
na bidhaa hapa nchini kupitia mchakato unaoendelea kupitia
mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook. Nafasi ya pili ilishikiliwa na
Kampuni ya mawasiliano ya Tigo na ya tatu kuchukuliwa na kampuni ya mawasiliano
ya Vodacom.
Katika mzunguko wa kwanza jumla ya makampuni 29 yaliingia katika
kinyanganyiro na kufanikiwa kuchukua ushindi katika makundi mbalimbali
.
Katika kundi la huduma za usafiri wa Anga , Shirika la Ndege la
Precision ndio liliongoza kwa kero na huduma zisizo na uhakika huku kundi la
huduma za maji likishikiliwa na Dawasco.
Kwa
upande wa usafiri wa mabasi Kampuni ya Happy Nation iliongoza kwa malalamiko
kutoka kwa wateja huku kundi la ving’amuzi vya Televisheni likiongozwa
na Star Times.
Kwa
upande wa huduma za maegesho ya magari , eneo la Magogoni Ferry limelalamikiwa
na wateja kwa huduma mbovu na kufanikiwa kushika nafasi za juu katika kundi
hilo.
Kwa
upande wa wateja wanaolipia huduma za Televisheni kituo cha TBC pekee ndicho
kimelalamikiwa kwa kutokuwa na huduma za uhakika kwa watazamaji wake.
Katika kundi la huduma za mawasiliano ya simu za mkononi , Kampuni ya
Tigo ndiyo iliibuka mshindi ikifuatiwa na Kampuni ya Vodacom.
Zoezi hili la kukusanya kero linafanywa na Wananchi
kupitia akaunti ya Twitter inayopatikana kupitia @hudumambayatz na
facebook group iliyopewa jina la HUDUMA BONGO ambapo huduma na bidhaa zote
zinazolipiwa na wateja mfano Burudani, Elimu, Hospitali, Hoteli, n.k
zinazowakera wateja zitaingia katika kinyanganyiro hicho.
Washauri wa kibiashara wa Huduma Bongo wanatoa wito kwa viongozi wa juu
wa Mashirika yote 29 yaliyotajwa kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha wateja
wao wanapata huduma bora kulingana na fedha wanazotoa ili kuweza kuleta
maendeleo ya Taifa.
Zoezi hili linaendelea ambapo katika mzunguko wa kwanza jumla ya kero
119 ziliwasilishwa na wateja endapo msomaji una kero iliyoshindwa kupatiwa
ufumbuzi na watoa huduma hawa unahitajika kuwa na akaunti inayotambulika ya
Twitter au Facebook na kujiunga na Huduma Bongo kisha ueleze kero yako. Ukweli
na Haki kuzingatiwa.
No comments:
Post a Comment