
Mohamed Seif Khatib

Dr Hussein Mwinyi

Shamsi Vuai Nahodha.

Omar Yussuf Mze
Samia Suluhu Hassan

Profesa Makame Mbarawa
MATOKEO ya uchaguzi wa wajumbe wa NEC katika kura
zilizopigwa juzi mjini Dodoma katika mkutano wa nane wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) yamevuja.
Huku
Mwenyekiti wa chama hicho kinachoiongoza Serikali, Rais Jakaya Kikwete
akitangaza jana kuwa matokeo hayo yatatangazwa leo pamoja na matokeo ya nafasi
za Makamu Mwenyekiti lakini tayari hadi jana mchana zaidi ya asiliamia 90 ya
wajumbe walisha jua matokeo hayo na kuanza kupongezana huku yale ya wagombea wa
bara yakiwekwa na idadi ya kura zao.
Ingawa baadhi ya wajumbe wameoneshwa kushangazwa na idadi ya kura alizopata Katibu Mkuu wa Chama hicho Wilson Mukama kwa kushika nafasi ya 9 huku Steven Wasira akiwaongoza.
Ingawa baadhi ya wajumbe wameoneshwa kushangazwa na idadi ya kura alizopata Katibu Mkuu wa Chama hicho Wilson Mukama kwa kushika nafasi ya 9 huku Steven Wasira akiwaongoza.
Wanaodaiwa kushinda nafasi 10 Zanzibar:
Mbunge wa Uzini, Mohamed Seif
Khatib; Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Ali Mwinyi, Waziri
wa Fedha Zanzibar, Omar Yussuf Mzee, Abdulhakim Chasama na Waziri wa
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha.Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Khadija Hassan Aboud, Bhaguanji Mansuria, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa na Khamis Mbeto.
No comments:
Post a Comment