ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 6, 2012

MKUTANO WA UMOJA WA WATANZANIA UJERUMANI NA WORLDMISSION SUNDAY 2012 WAFANA‏

Baadhi ya bidhaa za Tanzania katika meza za info.
Mhe. Ali Siwa kutoka Ubalozi wa Tanzania Ujerumani akiongea katika mkutano huo.

Wahisani wa Ujerumani wakiwa na Mhe. Ali Siwa na Mweneyekiti wa UTU, Bw. Mfundo (mwenye shati la bluu).
Kwa picha zaidi bofya read more
Mkutano ukiendelea.

Raia huyu wa Tanzania, Dogo Zeyra alikutwa akiwa kabeba mkoba wa mama yake baada ya mkutano kuisha.


-Wahisani washawishika zaidi kusaidia miradi Tanzania 
WATANZANIA walijumuika kwa wingi katika mkutano wa Worldmission Sunday uliofanyika Jumapili ya tarehe 28.10.12. 
Watanzania hao ambao walitoka pande mbalimbali za Ujerumani, walihudhuria mkutano huo ambao ulianza saa nne asubuhi mpaka saa 6 za mchana. Baada ya chakula cha mchana mkutano huo uliendelea hadi saa 12 za jioni.
Dk. Isaak Majura alitambulisha Taifa la Tanzania kwa kuonyesha Presentation ambayo ilitayarishwa na Jumuiya ya Watanzania Ujerumani (UTU).
Vilevile Katibu wa UTU alionyesha Presentation ya mradi wa shule ya msingi iliyopo maeneo ya Kigamboni Dar es Salaam ambapo wafadhili kadhaa walionyesha kushawishika sana na kutaka kujua ni jinsi gani wanaweza kuifikia shule hiyo ili kuangalia uwezekano wa kuchangia chochote katika maendeleo ya shule hiyo.
Mara baada ya kukamilika kwa presentation hizo, Mgeni Rasmi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Bw. Ali Siwa allitoa salamu rasmi kutoka Ubalozi wa Tanzania na kuwashukuru watayarishaji wa mkutano huo kwa upendo na mualiko kwa Umoja wa Watanzania Ujerumani.
Wakati huo huo, Bi. Tabia Mwanjelwa, (Muimbaji wa Maquiz wa Zamani) aliburudisha kwa kuimba na kupiga gitaa, ambapo aliwaacha hoi wafadhili waliohudhuria katika mkutano huo. Bi. Tabia Mwanjelwa alisema sauti yake na utaalamu wake wa kupiga gitaa ndio mchango wake kwa Watanzania.
Watayarishaji wa mkutano huo wamefurahishwa na wameridhika sana na mahudhurio ya Watanzania, pamoja na presentation zote mbili, na kuahidi kuwa Umoja wa Watanzania Ujerumani utapata mialiko mara kwa mara kunapotokea hafla za aina hii.
Umoja ni Nguvu!
kamati.utu@googlemail.com

No comments: