ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 14, 2012

MWIMBAJI WA WIMBO PAKA MAPEPE, MARIAM HAMISI AFARIKI DUNIA

MWIMBAJI nyota wa muziki wa Taarab, Mariam Khamis “Paka Mapepe” amefariki alfajiri ya jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mariam, ambaye hadi anafariki alikuwa ni mwajiriwa wa kundi la TOT Taarab, alipelekwa Muhimbili kwa ajili ya kujifungua lakini yeye akafariki na mtoto kutoka salama.
Kwa mujibu wa baba mdogo wa marehemu, Sembuli, Mariam atazikwa leo, na hilo ni ombi la Mkurugenzi wa kundi la TOT Kapteni John Komba kuomba hivyo ili na wao wahudhurie maziko ya mwenzao.
TOT iko Dodoma kwenye Mkutano Mkuu wa CCM.
Mariam alitamba na wimbo wa Paka Mapepe aliouimba akiwa na Melody, kabla ya kujiunga na Zanzibar Stars, Five Stars na hatimaye TOT.
Wimbo wake wa kwanza kurekodi na TOT ni Sidhuriki na Lawama ambao unatamba sana hadi leo hii.
Aidha msanii huyo akiwa Five Star alitamba na nyimbo za Uzushi wenu haunitii Doa na Ndio basi tena.
RIP

No comments: