BAINA MAZOLA NA MWAITE JUMA KUZIPIGA JUMAPILI
Bondia Baina mazola toka katika gym ya mzazi respect ya mabibo atazipiga na mtoto wa mwananyamala Mwaite Juma katika pambano lisilo la ubingwa la raundi nane.
pambano litakalofanyika katika ukumbi wa DID hall wa mabibo la kugombania kuwania kucheza ubingwa,kwani mshindi wa pambano hilo atakuwa na nafasi ya kucheza pambano la ubingwa na bondia bingwa wa uzito huo.
pambano hilo lililoandaliwa na kuratibiwa na Christopher mzazi lina lengo la kunyanyua vipaji vya mabondia chipukizi litawakutanisha mabondia wenye upinzani na uhasama toka sehemu mbalimbali ili wamalize kiu zao,kwani kuna baadhi ya vijana hao kuna waliofikia kupigana mitaani na wengine kurushiana maneno makali na kutishiana kuwa kila mmoja mbabe kwa mwenzake. hivyo wameandaliwa pambano wamalize bifu na kiu zao ili waendelee na mchezo kama mchezo kwa kunyanyua na kuendeleza vipaji vyao kwa manufaa yao kama ajira na maendeleo kwa taifa.
Katibu mkuu wa ngumi za kulipwa nchini IBRAHIM KAMWE amethibitisha kuwepo kwa pambano hilo na taratibu zote za mchezo wa ngumi zipo katika hatua ya mwisho kukamilikaa na mapambano ya utangulizi yatakuwa kama inavyoonesha hapo chini.
Date ;18/11/2012
Venue; D.I.D Hall-mabibo, Tanzania
Promoters; Bigright Promotion,Mzazi respect and 'no talking gym'
Matchmaker; Christopher "Mzaz'i
Bantam weight - MWAITE JUMA V/S BAINA MAZOLA 8 round
light fly - HERMAN SHEKIVULI V/S OMAR MAKUSUDI 4round
light fly - MARTIN RICHARD SHEKIVULI V/S SHOMARI PENDEZA 4round
light fly - ISSA OMAR V/S JAMES MARTIN 6round
wealter weight - ABDALAH LUWANJE V/S SAID MUHIDIN 6 round
light weight - mpole mackenzie v/s Adam Barnaba. 4 round
super fly - Shadrack juma v/s Ramadhan ustadh 4 round
Ngoyi Gaudence v/s Idd Mbishi 4 round
No comments:
Post a Comment