Mama Balozi Akipakwa Hina kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa elimuPics By Frank Eyembe
Mama Balozi akimkabidhi Mayorese Mrs. Anne Hobson baada ya kununua kitenge katika banda la Tanzania
Mama Balozi akiwaonyesha wageni Rasmi Mameya vitu mbalimbali vitakavyouzwa kwa ajili ya kuchangia mfuko huu.
Mama Kiondo akiwa kikazi zaidi kuitangaza Tanzania Pics
Mayorese Mrs. Anne Hobson katika banda la Tanzania
Mtahiki Meya akiangalia sehemu ya chakula ya Tanzania
Mtahiki Meya akifungua Tamasha
Sherehe ikiendeleaPics By Frank Eyembe.
Kwa picha zaidi bofya read more
Ukumbi wa Royal Borough of Kensington
kutoka Kushoto Mh balozi wa Grenada Ruth Elizabeth Rouse, Mtahiki Meya Christopher Buckmaster na Mama Balozi Joyce Kallaghe
wateja wakinunua bidhaa kutoka banda la Tanzania.
Jumuiya ya Commonwealth Countries League (CCL) inayoshirikisha nchi hamsini na nne (54) duniani kutoka katika jumuiya ya madola iliandaa tamasha maalum siku ya jumamosi tarehe 3.11.12 kwa ajili ya kuchangia mfuko wa kumsaidia na kumwezesha msichana kusoma elimu ya sekondari.
Historia ya Commonwealth Countries League ilianzishwa rasmi kutoka kwa baadhi ya wanawake mnamo mwaka 1923 nchini Australia kwa ajili ya kusaidia kutangaza uelewa wa haki sawa kati ya wanawake na wanaume waliopo nchi mbalimbali zilizo ndani katika jamuiya ya madola.
Tamasha hili lilifanyika Royal Borough of Kensington chini ya uongozi kutoka kwa Mh. Balozi wa Grenada Ruth Elizabeth Rouse ambaye ndio raisi wa jumuiya hiyo akisaidia na makamu wake mama Balozi Joyce Kallaghe. Wageni Rasmi walikua Wastahiki Mameya wa Worshipful Royal Borough of Kensington na Chelsea - Councillor Christopher Buckmaster na Mrs. Anne Hobson
Shughuli ya mwaka huu iliandaliwa na wake za mabalozi kutoka katika jumuiya za Madola hamsini na nne (54) ili kuchangisha pesa kwa njia ya kuuza vitu mbalimbali vya asili kama chakula, urembo, maua, vinywaji n.k. Fedha zote zilizopatikana zilipelekwa kusaidia mfuko huu wa Elimu kwa ajili ya kumsomesha mtoto wa kike.
Aidha Mama Balozi Joyce Kallaghe aliongeza kwa kusema ''Elimu ni Ufunguo Wa Maisha kumsomesha mwanamke ni kuiwezesha jamii nzima hivyo vipaumbele vyote vimeelekezwa kwa kwa ajili ya kuwasomesha watoto wa kike walio maskini au wanaoishi katika mazingira magumu ambao wana uwezo wa kuendelea kusoma elimu ya sekondari katika nchi za jumuiya ya Madola". Tangu mwaka 2011/2012 mfuko wa Elimu wa CCL ushawawezesha watoto wa kike 364 kutoka nchi 25 ikiwapo Tanzania. Pia aliwasihi wadau kuwa wazalendo kwa kuchangia mfuko huu kwa kuwasiliana kupitia barua pepe ccl.edfund@googlemail.com
Kiasi cha paundi mia moja hamsini (£150) na Mia nne na hamsini (£450) zinatosha kumsomesha msichana kwa mwaka mzima
Asanteni
Urban Pulse Creative











No comments:
Post a Comment