ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 12, 2012

Ushirikiano kati ya Tanzania na China wazidi kuimarika



Kaimu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Longinus  Rutasitara (katikati) akifafanua jambo wakati wa mkutano na Wajumbe  kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na wadau wengine (hawapo  pichani) kujadili misaada ya Serikali ya China katika kuisadia Tanzania 
kutekeleza miradi mikubwa katika sekta kama vile Kilimo, Miundombinu na  Umeme. Wengine katika picha ni Maafisa Waandamizi kutoka Tume hiyo.
Balozi Mbelwa Kairuki (kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia  katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akitoa mchango wake wakati wa majadiliano na ujumbe kutoka Serikali ya China kuhusu  kuisaidia Tanzania kutekeleza miradi yake mikubwa. Wengine katika picha 
ni Bw. Lin Zhiyong (katikati) Mwakilishi Mkuu katika masuala ya Uchumi  na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini na Bi.  Fang Wang, Afisa kutoka Ofisi hiyo.Picha na Habari-Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (Dar Yetu)

No comments: