Katibu wa Kamati ya kutetea haki za Waislamu,Sheikh Ponda Issa Ponda(katikati) na wenzake 49 wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu aliposomewa mashtaka ya uchochezi na kuvamia kiwanja kilichouzwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania(Bakwata) jijini Dar es salaam.
HATIMAYE washtakiwa wote katika kesi ya wizi na uchochezi inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wakati washtakiwa hao wakipewa dhamana, Sheikh Ponda ameendelea kubakia mahabusu kutokana na dhamana yake kufungwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP). Dhamana kwa washtakiwa hao ilitolewa baada ya wote kutimiza masharti .
Miongoni mwa masharti hayo, ni kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika, wenye vitambulisho na wote kusaini bondi ya dhamana ya Sh1 milioni.
Sambamba na masharti hayo, mahakama iliwapiga marufuku washtakiwa hao kwenda eneo la mgogoro uliowasababishia kesi hiyo (Markazi Chang’ombe) hadi kesi itakapokwisha.
Washtakiwa waliofikishwa mahakamani jana na kuachiwa kwa dhamana ni 30, ambao waliungana na wenzao 19 ambao walikuwa tayari wamepata dhamana kwa nyakati tofauti, baada kutimiza masharti hayo.
Sheikh Ponda na wenzake 49 walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Oktoba 18, mwaka huu chini ya ulinzi mkali na kusomewa mashtaka matano yakiwamo wizi na uchochezi.
Tuhuma zingine ni kula njama, kuingia kwa nguvu eneo lisilo mali yake kwa nia ya kutenda kosa, kujimilikisha ardhi kwa nguvu na kusababisha uvunjifu wa amani.
Mashtaka manne yanawahusu washtakiwa wote 50 isipokuwwa shtaka moja la uchochezi, ambalo linamhusu Sheikh Ponda pekee anadaiwa kuwashawishi wafuasi wake kutenda makosa ya uhalifu.
Wakati kesi hiy ilipotajwa mahakamani hapo Novemba Mosi, mahakama ilikubali kuwapa dhamana washtakiwa wote isipokuwa Sheikh Ponda ambaye mahakama ilisema haina mamlaka ya kisheria kwa kuwa DPP aliwasilisha hati ya kuzuia dhamana yake.
Siku hiyo Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi (SSA), Tumaini Kweka alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Siku hiyo Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi (SSA), Tumaini Kweka alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Hivyo, Kwaka aliomba mahakama ipange tarehe ya usikilizaji wa awali (PH), washtakiwa hao watasomewa maelezo ya awali ya kesi inayowakabili na kutakiwa kubainisha mambo wanayokubaliana na wasiyokubaliana nayo.
Hata hivyo, Wakili wa washtakiwa hao, Juma Nassoro alikumbusha mahakama kuhusu dhamana ya washtakiwa hao, akidai kuwa wakati walipopandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza, maombi yao ya dhamana hayakushughulikiwa kwa kuwa hakimu aliyepangwa kusikiliza kesi hiyo hakuwapo.
Hakimu Nongwa alikubaliana na maombi hayo ya dhamana na kusema dhamana iko wazi kwa washtakiwa wote, isipokuwa Sheikh Ponda ambaye dhamana yake imefungwa na DPP.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment