ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, December 9, 2012

Majambazi yateka gari lenye maiti na kupora

Msafara wa viongozi na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) cha Morogoro, uliokuwa unasafirisha mwili wa mwanafunzi wa chuo hicho umevamiwa na kutekwa na majambazi waliopora zaidi ya Sh. milioni 19 zikiwemo fedha za rambirambi, simu. kompyuta ndogo na mali nyingine za wasindikizaji.

Gari lililotekwa lilikuwa linatoka Morogoro kwenda Tarime mkoani Mara ni Toyota Land Cruiser namba SU 37012 lililokuwa na wanafunzi sita na viongozi wanne wa SUA wakisindikiza mwili wa mwanafunzi wa mwaka wa tatu, Munchari Lyoba. Mkasa huo ulitokea mkoani Singida.

Kwa mujibu wa mkuu wa msafara Makaranga Nonna, kabla ya majambazi hayo kupora wasindikizaji wanadaiwa kutumia mapanga, fimbo na kufyatua risasi hewani, kwa mujibu wa mkuu wa msafara Makaranga Nonna.

Akizungumza na NIPASHE Jumapili katika hospitali ya Mkoa Singida ulikohifadhi mwili wa marehemu Lyoba Nonna ambaye ni mfanyakazi wa SUA alisema mkasa huo ulitokea saa 7.30 usiku wa kuamkia jana.

Alisema, walipokaribia Singida mjini waliona mawe makubwa yakiwa yamewekwa barabarani, wakati dereva akijaribu kugeuza, ghafla kundi la majambazi lilizingira na kuanza kuvunja vioo vya gari lao kwa kutumia mawe lakini pia wakiwa na bunduki -magobore, na mashoka walianza kuwashambulia.

CHANZO:NIPASHE

No comments: