Wednesday, December 26, 2012

"Mr.Tz aanzisha msukumo wa kuleta curriculum mpya katika mfumo wa elimu wa Tanzania "



Mr TZ. Jumbe
Nafikiria kuanzisha msukumo wa kuleta curriculum mpya katika mfumo wa elimu wa Tanzania ambayo inalenga matatizo yanayoikabili Tanzania. Curriculum hiyo iwe ya kufundisha wanafunzi matatizo ya Tanzania na kujaribu kuyapatia ufumbuzi. Namna hiyo wanafunzi watajiona kuwa wamewezeshwa katika kubadili hali yao ya baadaye na mwelekeo wa taifa lao. Kwa hivi sasa hali ya baadaye ya wanafunzi, watu na Taifa lenyewe iko katika mikono ya serikali tu. Kama wanafunzi wote, ambao ni kundi kubwa Tanzania, watajifunza kuhusu matatizo yanayokabili taifa watataka kuchangia katika mabadiliko kwa sababu maisha yao ya baadaye yanategemea hali hiyo ya baadaye kwa taifa. Tunalenga wanafunzi kwa sababu ni kundi kubwa na wako tayari kujifunza mambo mapya. Toa mchango wako hapa, tushirikiane mawazo. Karibuni - Mr.Tz

http://www.facebook.com/PamojaWeCanReBuildTanzania?ref=hl

No comments: