ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 7, 2012

Ofisi ya kijiji yafungwa kwa miiba, M'kiti mbaroni


Na Martha Fataely, Moshi

WAKAZI wa Kijiji cha Kisangesangeni, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, wamefunga Ofisi ya kijiji kwa kutumia miba ya miti migumu ya migunga ili kuwashinikiza baadhi ya viongozi wa serikali ya kijiji hicho wajiuzulu.


Mbali ya kushinikiza wajiuzulu, wananchi hao wanataka viongozi husika wakamatwe kwa madai ya kuuza, kuhusika na uharibifu wa mazingira ya chanzo cha maji. 

Uamuzi huo ulifikiwa katika Mkutano Mkuu wa kijiji ambapo Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho, Bw. Musa Kabora, mbali 
ya kuwajibika kujiuzulu, alijikuta mikononi mwa polisi aliyemuita ili kuwadhibiti wananchi kwenye mkutano.

Wananchi hao walidai kuwa, chanzo hicho cha maji kimeuzwa sh. 800,000 kwa Mkandarasi iliaweze kuchukua udongo wa ujenzi wa mfereji wa umwagiliaji pamoja na kushinikizwa kukamatwa kwa viongozi wengine wa Serikali ya kijiji hicho Bw. Tadey Richard 
na Bw. Ali Mkindi.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwanasheria wa Halmashauri 
ya Wilaya hiyo, Bw. Baraka Chonya, alisema kuuza au kununua maeneo ya hifadhi ni makosa ambapo wote waliohusika sheria itachukua mkondo wake akiwemo mkandarasi.

Baada ya Bw. Chonya kutoa ufafanuzi huo, Bw. Kabora, aliamua kujiuzulu na kujikuta akikamatwa papo hapo.


Mbunge wa Vunjo, Bw. Augustine Mrema, amewapongeza wakazi wa kijiji hicho kwa kutekeleza agizo la Serikali ya mkoani huo la kuwaadhibu viongozi wanaohusika na uharibifu wa mazingira.

Alisema hatua hiyo ni ya kuigwa ili kujenga nidhamu ya uongozi ambapo viongozi watogopa kufanya matumizi mabaya.

No comments: