Uongozi wa jumuiya ya Watanzania waishio New York,New Jersey,Connecticut na Pennsylvania,unawatakia kheri ya Christmas na mwaka mpya wa 2013 wanajumuiya wote.Tunawaombea mwaka 2013 wenye kheri,upendo,busara,afya na mafanikio,sisi pamoja na ndugu,jamaa na marafiki zetu pamoja na marafiki wa jumuiya yetu.Tunamuomba Mwenyezi Mungu atulinde na atuepushe na mabalaa yote na pia atuongoze ili tuzidi kuwa wamoja,tuzidi kupendana,kushauriana,kusaidiana,kuaminiana,kushirikiana na kuongozana ili tujenge jumuiya ya Watanzania yenye nguvu kwani umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
Uongozi wenu pia hauna budi kuwashukuru wanajumuiya wote walioshiriki katika kuijenga,kuiendeleza,kuisaidia,kuilea na kuisimamia jumuiya yetu kwa kipindi chote cha mwaka 2012.Pamoja na misukosuko ya kimbunga Sandy(Hurrican Sandy) na mitihani mengine mingi ya kimaisha,Watanzania kwa pamoja tuliungana na kwa uwezo wa Menyezi Mungu tuliweza kuishinda mitihani hiyo kwa pamoja.Uongozi pia hauna budi kuwapa mkono wa faraja wanajumuiya wote waliopoteza wapendwa wao na misiba iliyotusibu na tuzidi kumuomba Mwenyezi Mungu atupe nguvu na atusahaulishe na pia awape makazi mema ya milele marehemu wetu. Mungu ubariki umoja wetu,Mungu ibariki Tanzania. Ameen!
Marry X-Mass and Happy New Year!
Hajji Khamis
Mwenyekiti
NYTC.
No comments:
Post a Comment