Wednesday, December 26, 2012

SHUKURANI ZA DHATI


Ndugu wapendwa
Kwa niaba ya ndugu yetu Richard Mwandemani (DJ Rich Maka) familia yake, ndugu na jamaa, tunapenda kutoa  shukran zetu za dhati kwa ushirikiano mwema mliouonyesha toka mzee wetu Edson Mwandemani alipokuwa amelazwa hospitali kwa kuja kumjulia hali hadi  kilio kilipotokea  jinsi mlivyoshughulika kwa misaada yenu ya hali na mali.Hatuna cha kuwalipa ila Mwenyezi Mungu mwenyewe atawalipa malipo yalio stahili.
 Mwili wa marehemu mzee Mwandemani utaondoka Ijumaa tarehe 28 December, 2012 kwa safari ya kwenda nyumbani na kufika Tanzania Jumapili  jioni December 30, 2012.
Asanteni sana na shukrani kwa wema na ukarimu wenu.

Isaac Kibodya, kwa niaba ya Richard Mwandemani  (DJ Rich Maka) na familia yake.

No comments: