ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 17, 2012

SHUKURANI ZANGU ZA DHATI


.Natoa shukrani zangu kwa Watanzania wenzangu kaka zangu na dada zangu wote kwakweli mmenionyesha upendo wenu na ushirikiano wenu mkubwa nawashuru sana sana umoja ni nguvu vivaa california.

Nilifika salama DC moyo mlionionyesha naomba uelendelee kwa mwingine yeyote mwenye nia na uzalendo kuonyesha ujuzi aliokua nao kwa Watanzania wenzake.

Upendo wenu umenifanya nijisikie kwamba siko peke yangu kwenye Dunia ya California daima mpo juu. Ninaipenda sana hii kazi ya ubunifu na ndio maana mliponihitaji sikusita hata chembe kuja huko kwa kujua, kutambua na kuthamini umuhimu wa hii sherehe ya miaka 51 ya Uhuru na kwamba ujio wangu huko utanogesha sherehe ya uhuru na kufungua njia mpya ya uhusiano wangu na Watanzania wa California.

Najua mtajiuliza kwanini nimechelewa kutoa hizi shukurani, kusema ukweli ukarimu wenu ulinifanya nisijue wapi pa kuanzia kuandika shukurani zangu.

Napenda kumshukuru Asya Idarous Khamsin kwa kutambua kipaji changu pia nitakua mchoyo wa fadhila nisipo mshukuru Walter Minja kwa kutambua juhudi nazofanya kuendeleza hii sanaa ya ubunifu Pia nawashukuru sana Emmanuel na mkewe, bila kumsahau Esther.

Asante sana California nawapenda sana Mwenyezi Mungu awabariki sana.

KWETU Fashion Design By Missy Temeke

2 comments:

Anonymous said...

Missy Temeke,,

Kipaji chako cha ubunifu ni pekee. Mola akuzidishie zaidi

Walter

Anonymous said...

Miss Temeke ni kweli amejaaliwa na Mungu na kipaji chake ni kweli ni cha kipekee,hongera sana na ongeza bidii kila mtu mdomoni ni Miss Temeke kwa sifa zake tunazozipokea.