Tunapenda kutoa shukurani zetu za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa kuacha shughuli zenu na kujumuika nasi katika wakati wetu mgumu wa maombolezo, malewazo, maombi na sala za kumrehemu mpendwa wetu Bi. Helena Jonathan Mnguto (mama mzazi wa Felix Mnguto).
Tumefarijika sana kwa ushirikiano wa hali na mali tulioupata kutoka kwenu nyote.
Salamu zenu tumezifikisha kwa Bw. John Mnguto (mume wa marehemu) pamoja na familia yake huko Tanga, Tanzania.
Mwenyezi Mungu aendelee kuwajaza na upendo.
Amen.
Familia ya Felix Mnguto, akishirikiana na uncle Sichele, aunty Esther, akina Kalala na akina Nyang'oro
No comments:
Post a Comment