TAASISI ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Morogoro, imewafikisha mahakamani wafanyakazi watatu wa wakala wa Barabara Nchini (TANRODS) wa kituo cha mizani cha Mikese mkoani hapa kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Sh40,000.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mkuu wa taasisi hiyo Mkoa wa Morogoro, Stella Mpanju tukio la kuwafikisha katika mahakama ya wilaya ya Morogoro watuhumiwa hao lilifanyika Desemba 13 ambapo kesi ilitajwa kwa mara ya kwanza na inatarajiwa kusikilizwa tena leo.
Mpanju alisema watuhumiwa hao ambao ni Happiness Minja (29), Victor Mongi (30) na Eliud Mwakamela (29) walifikishwa mahakamani hapo baada ya kuvunja sheria ya kutoa na kupokea rushwa kifungu cha 15 (10)(a) namba 11 ya mwaka 2007.
Alisema washtakiwa hao walikamatwa Desemba 10, baada ya mshtakiwa kwanza, Happiness Minja, kudaiwa kuomba hongo ya Sh40,000 kutoka kwa dereva wa lori ambalo lilikuwa limezidisha uzito na fedha hizo kudaiwa kugawiwa kwa wafanyakazi wote watatu.
Kutokana na tukio hilo mkuu huyo wa TAKUKURU Mkoa wa Morogoro ametoa wito kwa wananchi hususan madereva kutoa taarifa za vitendo vya rushwa vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wasio waadilifu wa mizani za Mikese, Kihonda na Mikumi ili hatua ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
MWANANCHI
1 comment:
It is so strange that Takururu would arrest and prosecute criminals for a theft of only $20 (or 40,000Tshs) while leaving free the accursed of billions or rather, trillions of US.Dollar stolen and kept abroad. Hosea, this is kidding, please!
Post a Comment