Advertisements

Tuesday, January 22, 2013

BALOZI WA UINGEREZA AMTEMBELEA KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA JIJINI DAR

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na mgeni wake, Balozi wa Uingereza hapa nchini, Diane Corner, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na kulia ni Mkuu wa Mawasiliano na Siasa wa Ubalozi huo, Mark Polatajko.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Balozi wa Uingereza hapa nchini, Diane Corner aliyemtembelea leo, Januari 22, 2013, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo maalum ya kikazi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Diane Corner, baada ya mazungumzo yao, leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na kulia ni Mkuu wa Mawasiliano na Siasa wa Ubalozi huo, Mark Polatajko.

(Picha Zote na Bashir Nkoromo).

No comments: