ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 29, 2013

DHAMANA YA LULU YAKAMILIKA PATA TASWIRA

Lulu na mama yake mzazi wakilia baada ya kukutana nje ya Mahakama, Lulu ameachiwa huru na Mahakama leo january 29 2013 mchana, pembeni ni mwigizaji Dr. Cheni ambae amekua karibu na familia ya Lulu kwa muda mrefu sana.
Lulu akiingia kwenye gari.
Machozi ya furaha.


Lulu akiondoka mahakama hapo.



Wakili anayemtetea Lulu akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya mteja wake kupata dhamana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo. Lulu amepata dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali waliosaini bondi ya Sh.milioni 20 kila mmoja, kusalimisha hati ya kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam bila ruhusa ya mahakama na kuripoti kwa msajili kila mwezi. Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba.

No comments: