ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 15, 2013

KUMBUKUMBU

Leo Januari 15 ni mwaka mmoja tangu mama yetu mpendwa Anna Ng'weshemi ulipotutoka. Ilikuwa tarehe 15/1/2012 siku ambayo familia yetu pamoja na marafiki zetu tulijawa huzuni na majonzi baada ya wewe mama yetu kuondoka na kutuacha peke yetu katika dunia hii. Mama, sisi watoto wako, wajukuu zako na kizazi chako chote tunasema kwamba ingawa kimwili hauko nasi katika dunia hii lakini mioyo, akili na mawazo yetu viko pamoja na wewe mbinguni ambapo tunaamini kuwa Mungu amekupumzisha. Tunakukumbuka na daima tutakukumbuka.
BWANA ALITOA NA PIA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.



No comments: